“Julai 27–Agosti 2. ‘Ninafanya Kazi Kuu”: Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Julai 27–Agosti 2. ‘Ninafanya Kazi Kuu,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Nina Kazi Kubwa ya Kufanya, na Tyson Snow
Julai 27–Agosti 2: “Ninafanya Kazi Kuu”
Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8
Wayahudi walikuwa wamechukuliwa mateka katika Babeli kwa takribani miaka 70. Walikuwa wameipoteza Yerusalemu na hekalu, na wengi walikuwa wamesahau ahadi zao katika sheria za Mungu. Ila Mungu hakuwa amewasahau wao. Kimsingi, Yeye alikuwa ametangaza kupitia manabii Wake, “Nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa” (Yeremia 29:10). Mkweli kwa unabii huu, Bwana aliweka njia kwa watu Wake kurudi—kote Yerusalemu na, muhimu zaidi, kwenye maagano yao. Na yeye aliwainua watumishi walioikamilisha “kazi kubwa” (Nehemia 6:3): Gavana aliyeitwa Zerubabeli alisimamia ujenzi wa nyumba ya Bwana. Ezra, kuhani na mwandishi, aliwasaidia watu kuigeuza mioyo yao kurudi kwenye sheria ya Bwana. Na Nehemia aliongoza ujenzi wa kuta za ulinzi kuzunguka Yerusalemu. Walikutana na upinzani, lakini pia walipata msaada kutoka vyanzo visivyotarajiwa. Uzoefu wao unaweza kutufahamisha na kutupa misukumo, kwa sababu sisi pia tunafanya kazi kubwa. Na kama kazi yao, kazi yetu ina mengi ya kufanya kuhusiana na nyumba ya Bwana, sheria ya Bwana, na ulinzi wa kiroho tunaoupata Kwake.
Kwa ajili ya muhtasari wa vitabu vya Ezra na Nehemia, ona “Ezra” na “Nehemia” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ezra 1
Bwana huwapa misukumo watu kutimiza makusudi Yake.
Baada ya Uajemi kuishinda Babeli, Bwana alimpa ushawishi Mfalme wa Uajemi, Koreshi, kutuma kundi la Wayahudi Yerusalemu ili kujenga upya hekalu. Unaposoma Ezra 1, angalia kile ambacho Koreshi alifanya ili kuwaunga mkono Wayahudi katika kazi hii muhimu. Ni kwa jinsi gani unamwona Bwana akifanya kazi kupitia wanaume na wanawake wanaokuzunguka, ikijumuisha watu ambao si waumini wa Kanisa? Hii inapendekeza nini kwako kuhusu Bwana na kazi Yake?
Ona pia Isaya 44:24–28.
Ezra 3:8–13; 6:16–22
Nyumba ya Bwana ni nyumba ya shangwe.
Wakati Wababeli walipoivamia Yerusalemu, walipora na kuchoma hekalu na kuliteketeza kabisa (ona 2 Wafalme 25:1–10; 2 Mambo ya Nyakati 36:17–19). Unafikiri ungejisikia vipi kama ungekuwa mojawapo wa Wayahudi walioshuhudia hili? (ona Z\aburi 137). Gundua jinsi Wayahudi walivyohisi, miongo mingi baadae, wakati waliporuhusiwa kurudi nyumbani na kujenga upya hekalu (ona Ezra 3:8–13; 6:16–22). Hiyo inaweza kukupa msukumo kutafakari hisia zako mwenyewe kuhusu Bwana na nyumba Yake. Kwa nini ujenzi wa hekalu ni sababu ya kusherehekea?
Hekalu la Zerubabeli, kielelezo na Sam Lawlor
Ezra 4–7; Nehemia 2; 4; 6
Mungu ana kazi muhimu ya kufanywa nami.
Kazi ya Bwana mara chache huenda bila upinzani Hii ilikuwa kweli juu ya juhudi zilizoongozwa na Zerubabeli na Nehemia. Hapa kuna njia rahisi ambayo inaweza kukusaidia kujifunza kutoka kwenye hadithi hizi na kufikiria jinsi unavyoweza kufanya kazi ya Bwana licha ya upinzani:
Kazi ya Mungu kwa ajili ya Zerubabeli (Ezra 4:3):
Kazi ya Mungu kwa ajili ya Nehemia (Nehemia 2:17–18):
Kazi ya Mungu kwa ajili yangu:
Upinzani ambao Zerubabeli alikabiliana nao (Ezra 4:4–24):
Upinzani ambao Nehemia alikabiliana nao (Nehemia 2:19; 4:1–3, 7–8; 6:1–13):
Upinzani ninaokabiliana nao mimi:
Jinsi Zerubabeli alivyojibu (Ezra 5:1–2):
Jinsi Nehemia alivyojibu (Nehemia 2:20; 4:6, 9; 6:3–15):
Jinsi mimi ninavyoweza kujibu:
Kwa usaidizi wa hulinganisha uzoefu wa Nehemia na maisha yako, ungeweza kujifunza ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “We Are Doing a Great Work and Cannot Come Down” (Liahona, Mei 2009, 59–62), hususani sehemu mbili za mwisho. Unapofikiria kuhusu kazi ambayo Mungu amekupa, unaweza kujifunza “Dhima ya Wasichana” au “Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni” (Gospel Library). Au mngeweza kuangalia katika wimbo kama “Dada wa Sayuni” (Nyimbo za Dini, no. 169) or “Wazee wa Israeli” (Nyimbo za Dini, no. 170).
Je, unafikiria inamaanisha nini kuwa na “moyo wa kufanya kazi” katika huduma ya Mwokozi? (Nehemia 4:6). Inaweza kumaanisha nini kuwa na “mkono mzuri wa … Mungu juu [yako]” unapofanya kazi Yake? (Nehemia 2:8; ona pia Nehemia 2:18; Ezra 7:6, 9, 27–28). Ni kwa jinsi gani umeuona mkono Wake katika juhudi zako za kumtumikia Yeye?
Nehemia 8
Ninabarikiwa wakati ninapojifunza maandiko.
Kwa vizazi katika utumwa, Wayahudi walikuwa na uwezo mdogo wa kukifikia “kitabu cha sheria ya Musa” (Nehemia 8:1). Katika Nehemia 8, Ezra aliwasomea watu sheria. Unapata nini katika sura hii ambacho kinaonyesha jinsi Ezra na watu wake walivyohisi kuhusu Mungu na neno Lake? (ona hususani mistari 1–12). Ni kipi katika maisha yako kinaonyesha jinsi unavyohisi kuhusu Mungu na neno Lake?
Ona pia Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley (2014), 115–24.
Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ezra 3:8–13; 6:16–22
Nyumba ya Bwana ni nyumba ya shangwe.
-
Ili kuwafundisha watoto wako kuhusu shangwe ambayo Wayahudi walihisi wakati hekalu lao lilipojengwa upya, ungeweza kuwaonyesha wao picha kama ile iliyopo hapa chini. Zungumza kuhusu kwa nini watu hawa wanaweza kuwa na furaha kuwa katika nyumba ya Bwana. Ungeweza pia kuwaambia watoto wako kwa nini hekalu ni mahali pa shangwe kwako. Je, hekalu limekusaidia vipi kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni na Mwokozi?
-
Unaposoma Ezra 3:10–13 pamoja na watoto wako, wasaidie watafute maneno ambayo yanaonyesha jinsi Wayahudi walivyohisi wakati hekalu lilipokuwa likijengwa upya. Mnapofika mwisho wa mstari wa 13, pengine mngeweza kupiga kelele kwa shangwe pamoja. Wasaidie watoto wako wafikirie sababu za kuwa na shangwe kwamba Bwana ametupatia mahekalu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha shangwe hiyo?
-
Fikiria kuimba wimbo kuhusu hekalu pamoja na watoto wako, kama vile ubeti wa pili wa “Karibu Nyumbani” (Maktaba ya Injili). Baada ya kila mstari, ungeweza kutua na kumuomba mtoto ashiriki kitu fulani anachokipenda kuhusu hekalu. Unaweza pia kuangalia picha za mahekalu wakati mkiimba.
Nehemia 2:17–20; 6:1–9
Bwana atanisaidia kufanya “kazi Yake kubwa.”
-
Shiriki na watoto wako hadithi ya Nehemia (ona Nehemia 2:17–20; 6:1–9; au “Nehemia” katika Hadithi za Agano la Kale, 173–74). Unaposoma Nehemia 2:20, wewe na watoto wako mngeweza “kuinuka” na kujifanya kusaidia kujenga kuta za Yerusalemu. Au watoto wako wangeweza kufurahia kujenga ukuta kwa kutumia matofali au vitu vingine. Wanapofanya hivyo, ungeweza kuwasaidia kufikiria juu ya vitu muhimu ambavyo Baba wa Mbinguni anatutaka tufanye.
1:38Nehemiah
-
Unaposoma Nehemia 6:9, waalike watoto wako wainue mikono yao wakati wanaposikia ukisema “imarisha mikono yangu.” Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulihisi Mungu akiimarisha mikono yako kufanya kazi Yake.
Nehemia 8:1–12
Maandiko ni baraka.
-
Soma kwa sauti virai kutoka Nehemia 8:2–3, 5–6, 8–9, 12 ambavyo vinaeleza kile watu walichofanya waliposikia maandiko, na uwaalike watoto waigize virai. Unaposoma, watoto wako wangeweza kuigiza virai hivi. Kisha mngeweza kushiriki na kila mmoja jinsi mnavyohisi wakati mnaposoma au kusikia maandiko.
-
Mnaposoma pamoja Nehemia 8:8, ungeweza kuwauliza watoto wako ni nini kinawasaidia kuelewa maandiko. Waoneshe jinsi ya kutumia visaidizi vya kujifunza maandiko kama Mwongozo wa Maandiko na Mada na Maswali (Maktaba ya Injili). Waalike watoto wako washiriki kitu walichojifunza kuhusu Mwokozi kutoka kwenye maandiko.
Tafuta ukweli wa milele katika maandiko. “Maandiko … yamejazwa kweli za injili, lakini wakati mwingine inahitaji jitihada ya dhati kuzipata. Mnapojifunza pamoja kutoka kwenye maandiko, tua kidogo na waulize wale unaowafundisha ni ukweli gani za injili wameziona. Wasaidie waone jinsi kweli hizi zinavyohusika kwenye mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Wakati mwingine kweli za milele zimeelezwa katika maandiko, na wakati mwingine zimefafanuliwa katika hadithi na maisha ya watu tunaosoma habari zao. Inaweza pia kuwa ya msaada kuchunguza pamoja historia ya mistari unayoisoma, vile vile maana ya mistari hiyo na jinsi inavyotumika kwetu sisi leo” (Katika Njia ya Mwokozi, 22).
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .