Juni 29–Julai 5. ‘Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni Yeye’: 1 Wafalme 12–13; 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
Juni 29–Julai 5. ‘Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Eliya Anabishana dhidi ya Makuhani wa Baali, na Jerry Harston
Juni 29–Julai 5: “Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni”
1 Wafalme 12–13; 17–22
Nyumba ya Israeli ilikuwa katika vurugu. Ufalme wa ulikuwa umegawanyika, kukiwa na makabila kumi yakiunda Ufalme wa Kaskazini wa Israeli na makabila mawili yakiunda Ufalme wa Kusini wa Yuda. Lakini kibaya zaidi kuliko utengano wao kutoka kwa kila mmoja ilikuwa ni utengano wa falme kutokana na maagano yao. Wafalme waovu waliwaongoza watu mbali na Bwana, na watu wengi waliyumba katika imani yao.
Katika mazingira haya, Bwana alimwita Eliya kuwa nabii. Maisha yake yanaonyesha kwamba mtu anaweza kuwa na imani kubwa katika Bwana hata katika hali mbaya. Wakati mwingine Bwana anajibu kwenye imani kama hiyo kwa miujiza ya kuvutia na ya hadharani, kama kushuka kwa moto kutoka mbinguni. Lakini Yeye pia hufanya miujiza ya kimyakimya na binafsi, kama kulisha mjane mwaminifu na mwanawe. Na mara nyingi miujiza Yake ni ya binafsi kwamba inajulikana kwako tu mtu mmoja—kwa mfano, wakati Bwana anapojidhihirisha Mwenyewe na mapenzi Yake kupitia “sauti ndogo, ya utulivu” (1 Wafalme 19:12).
Kwa mengi kuhusu Eliya, ona “Eliya” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
1 Wafalme 12:1–20
Viongozi wenye haki huwabariki watu wanaowaongoza.
Ni kwa jinsi gani ungeelezea kosa ambalo Mfalme Rehoboamu, mwana wa Sulemani, alifanya katika 1 Wafalme 12:1–14? Ni sifa zipi kama za Kristo zingeweza kumsaidia Rehoboamu kuokoa ufalme wake? (ona mstari wa 7; Mathayo 20:25–28; Mosia 2:10–21). Unawezaje kutumia sifa hizi kama kiongozi—iwe katika wito wa Kanisa au kama kiongozi wa maisha yako mwenyewe?
1 Wafalme 17:8–16; 19:19–21
Mwaliko wa kutoa dhabihu ni nafasi ya kutumia imani yangu katika Yesu Kristo.
Nabii Eliya alimwomba mjane ampe yeye chakula na maji kabla ya kujilisha mwenyewe na mwanawe mwenye njaa. Kwa nini angefanya hivyo? Ombi la Eliya lingeweza pia kuonekana kama baraka kwa familia hii ndogo. Walihitaji baraka za Bwana, na dhabihu huleta baraka—ikiwa ni pamoja na baraka ya imani thabiti.
Unaposoma 1 Wafalme 17:8–16, fikiria kuwa wewe ulikuwa mjane huyu. Nini kinachokuvutia kuhusu yeye? Ungeweza pia kutengeneza orodha ya chaguzi ambazo zinahitaji imani katika Yesu Kristo (kwa mifano, ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi [2022]). Unajifunza nini kutoka kwa mjane huyu kuhusu kutumia imani?
Ni kwa jinsi gani matendo ya Elisha katika 1 Wafalme 19:19–21 yanafanana na matendo ya mjane?
Fikiria kuhusu dhabihu ulizofanya ili kumfuata Mwokozi. Je, 1 Wafalme 17:8–16; 19:19–21 i inakufundisha nini kuhusu dhabihu hizi? Ni jinsi gani uelewa juu ya Mwokozi unakusaidia wewe wakati anapokuomba kutoa dhabihu? Je, Yeye amekubariki vipi?
Ona pia Mathayo 4:18–22; 6:25–33; Luka 4:24–26; “Elijah and the Widow of Zarephath” (video), Maktaba ya Injili; “When Faith Endures,” Nyimbo za Dini, na. 128.
Elijah and the Widow of Zarephath
1 Wafalme 18
“Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni.”
Waisraeli wangeweza kuhisi walikuwa na sababu nzuri za kumwabudu Baali, ambaye alijulikana kama mungu wa dhoruba na mvua. Baada ya miaka mitatu ya ukame, walihitaji sana mvua. Na kumwabudu Baali ilkuwa imekubalika kijamii na kutangazwa na mfalme na malkia. Unaposoma 1 Wafalme 18, fikiria ni kwa nini mtu katika siku yetu anaweza kuwa asiye na maamuzi kuhusu kumfuata Bwana. Katika sura hii, unafikiri Bwana alikuwa anajaribu kufundisha nini kuhusu Yeye mwenyewe? Ni uzoefu gani umekusaidia kuamua kumfuata Mwokozi?
Ona pia D. Todd Christofferson, “Choice and Commitment” (worldwide devotional for young adults, Jan. 12, 2020), Gospel Library.
Kielelezo cha Eliya, na Wilson Ong
1 Wafalme 19:1–18
Bwana mara nyingi huzungumza katika njia za utulivu, na rahisi.
Cha kusikitisha, muujiza kwenye Mlima Karmeli haukufanya misheni ya Eliya kuwa rahisi. Kwa kweli, maisha yake yalikuwa hatarini, na ilibidi ajifiche ndani ya pango huko nyikani. Hapo, akipambana na upweke na kukata tamaa, alikuwa na uzoefu na Bwana ambao ulikuwa tofauti na kile kilichokuwa kimetokea juu ya Mlima Karmeli. Uzoefu wa Eliya katika 1 Wafalme 19:1–18 unakufundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyowasiliana na wewe katika wakati wako wa uhitaji?
Tafakari nyakati ambapo unahisi Bwana amezungumza nawe. Ni kwa jinsi gani ungeelezea jinsi Yeye anavyowasiliana nawe? Kwa nini maneno “tulivu” na “ndogo” ni njia nzuri za kuelezea sauti ya Roho? Ni maneno gani mengine unayoyapata katika Helamani 5:30; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 11:12–14? Je, unahitaji kufanya nini ili kupokea mwongozo wa Bwana kila mara?
Ona pia Zaburi 46:10.
Tumia milango mingi ya fahamu ili kuboresha kujifunza. Sote tunajifunza kuhusu ulimwengu kupitia njia zetu tano za ufahamu. Kwa kutumia njia hizo tunaweza pia kuboresha kujifunza injili. Kwa mfano, fikiria picha au sauti ambazo ungeweza kutumia kuonesha maneno “tulivu” na “ndogo” unapojifunza au kufundisha kuhusu sauti ya Bwana katika 1 Wafalme 19.
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
1 Wafalme 17
Bwana hunibariki ninapokuwa na imani Kwake.
-
Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze hadithi za imani katika 1 Wafalme 17, ungeweza kuwaonyesha picha au vitu ili kuelezea hadithi, kama vile ndege, mkate, au mvulana. Unapowaelezea watoto wako hadithi hizi, waalike watafute picha au kitu ambacho kinaendana na kila hadithi. “Eliya Nabii” (katika Hadithi za Agano la Kale, 121–24) inaweza kukusaidia kusimulia hadithi hizi. Je, kila hadithi inatufundisha nini kuhusu kuwa na imani katika Yesu Kristo?
1:58Elijah the Prophet
-
Wasaidie watoto wako wafikirie njia wanazoweza kuonyesha imani yao katika Yesu Kristo. Imba pamoja nao wimbo kuhusu imani, kama vile “I Have Faith in the Lord, Jesus Christ” (Maktaba ya Injili), na shiriki na kila mmoja kile unachojifunza kuhusu imani kutoka kwenye wimbo.
Kielelezo cha Eliya na uponyaji wa mwana wa mjane, na Charles Edmund Brock
1 Wafalme 17:8–16
Wakati Bwana anaponiomba nifanye dhabihu, ninaweza kutii kwa imani.
-
Pengine watoto wako wangeweza kuchora picha ya kile Bwana alichomwomba mjane kumpa Eliya (ona 1 Wafalme 17:12–13) na kile mjane alichopokea kama malipo (ona 1 Wafalme 17:15–16). (Ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii.) Wangeweza pia kutafuta picha za watu wengine ambao waliacha kitu fulani walichokitaka kwa ajili ya kitu bora zaidi. Waalike watoto wako watafute picha katika Kitabu cha Sanaa ya Injili au Njoo, Unifuate. Je, Bwana anatuomba sisi tutoe dhabihu ya nini? Ni kwa jinsi gani Yeye anatubariki sisi?
1 Wafalme 18:17–39
Ninaweza kuchagua kumfuata Yesu Kristo.
-
Mnaposoma 1 Wafalme 18:17–39 pamoja, watoto wako wangeweza kuchagua mstari na kuchora picha ya kile inachoelezea. Wangeweza kutumia picha zao kuelezea hadithi katika maneno yao wenyewe. (Ona pia “Eliya na Makuhani wa Baali,” katika Hadithi za Agano la Kale, 125–28.)
2:17Elijah and the Priests of Baal
-
Wasaidie watoto wako wafikirie juu ya hali wakati watakapohitajika kuamua ama au sivyo kumfuata Yesu Kristo. Pengine wangeweza kuchora picha zao wenyewe wakifanya uchaguzi sahihi. Shiriki na kila mmoja kwa nini unachagua kumfuata Yesu.
1 Wafalme 19:9–12
Bwana huongea nami kupitia sauti ndogo, tulivu ya Roho Mtakatifu.
-
Unapofanya muhtasari wa 1 Wafalme 19:9–12, waalike watoto wako wafanye vitendo kuwakilisha upepo mkali, tetemeko la ardhi, na moto. Kisha waalike wakae wametulia kabisa unaposema pamoja kwa sauti tulivu, “baada ya moto sauti ndogo ya utulivu” (mstari wa 12) (Ona pia “Bwana Anazungumza na Eliya,” katika Hadithi za Agano la Kale, 129–31.) Waambie watoto wako kuhusu nyakati ambapo umepata uzoefu wa sauti tulivu, ndogo ya Roho Mtakatifu.
1:48The Lord Speaks to Elijah
-
Kwa ukimwa imbeni wimbo kuhusu Roho kama vile “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106–7). Ni nini kinaweza kutuvuruga tusiweze kumtambua Roho? Ni nini kinaweza kutusaidia kumsikiliza Yeye?
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .