Njoo, Unifuate
Juni 22–28. “Uyasikie huko Mbinguni Maombi Yao”: 2 Samweli 11–12; 1 Wafalme 3; 6–9; 11


“Juni 22–26. ‘Uyasikie huko Mbinguni Maombi Yao’: 2 Samweli 11–12; 1 Wafalme 3; 6–9; 11,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Juni 22–26. ‘Uyasikie huko Mbingni Maombi Yao,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Sulemani akiweka wakfu hekalu

Sulemani Anaweka Wakfu Hekalu Yerusalemu, na James Tissot na wengine

Juni 22–28: “Uyasikie huko Mbingni Maombi Yao”

2 Samweli 11–12; 1 Wafalme 3; 6–911

Sauli, Daudi, na Sulemani, wafalme watatu wa kwanza wa Israeli, wote walianza kwa ahadi nyingi. Wanyenyekevu, jasiri, na wenye hekima, kila mmoja alipata neema kwa Bwana—angalau mwanzoni. Cha kuhuzunisha, kila mfalme pia aliangushwa na udhaifu wa kibinadamu na majaribu. Waliweka matamanio yao wenyewe mbele kuliko ya Bwana. Na kama tulivyoona tena na tena katika maandiko—na katika maisha yetu wenyewe—hiyo ilisababisha janga.

Lakini kitu fulani muhimu kilitokea wakati wa utawala wa Sulemani ambacho kilitoa tumaini fulani kwa utengemano katika maisha ya watu wa agano. Sulemani alijenga hekalu. Ilikuwa ni nyumba ya kudumu zaidi ya Bwana kuliko tabenakulo ilivyokuwa. Na ingewakilisha uwepo wa kudumu zaidi wa Bwana miongoni mwa watu Wake. Sulemani alijua kwamba watu wangeendelea kukabiliana na udhaifu na majaribu ya aina mbalimbali. Katika kuweka wakfu nyumba hiyo mpya takatifu, Sulemani alimsihi Bwana, “Kama wao … watakaporejea kwako kwa mioyo yao yote, … basi uyasikie maombi yao” (1 Wafalme 8:47–48). Hiyo ni sehemu ya kile ambacho maagano ya hekaluni hufanya kwa ajili yetu—yanatengeneza muunganiko na Mungu. Yanapata kwa ajili yetu ahadi kwamba kupitia toba yetu na rehema Yake, Yeye anaweza “kukaa miongoni [mwetu]” na kamwe hatatuacha (1 Wafalme 6:13).

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha 1 Wafalme, ona “Wafalme, vitabu vya” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

2 Samweli 11; 12:1–14

ikoni ya seminari
Bwana anaweza kunisaidia kufanya chaguzi nzuri wakati ninapojaribiwa kutenda dhambi.

Wakati mwingine tunawatazama watu wanaoonekana kuwa imara katika imani yao, na tunadhani kwamba hawaathiriwi na majaribu. Chaguzi za kusikitisha za Daudi zilizoelezewa katika 2 Samweli 11 zinaonyesha wazi kwamba hii sio hviyo. Fikiria somo unaloweza kujifunza kutokana na uzoefu wake. Maswali kama haya yanaweza kukusaidia kujifunza 2 Samweli 11–12:

  • Ni chaguzi zipi Daudi alizifanya ambazo zilimwongoza chini kwenye njia ya ongezeko la dhambi? Ni chaguzi zipi za haki angeweza kufanya badala yake? (Ona pia video “To Look Upon” Gospel Library).

    4:15

    To Look Upon

    Kutumia video. Video zinaweza kukusaidia kupata taswira ya maelezo kutoka kwenye maandiko na kuzingatia jinsi yanavyotumika kwako. Fikiria jinsi unavyoweza kuzitumia ili kuboresha kufundisha na kujifunza. Kwa mfano, wakati ukitazama “To Look Upon” (Gospel Library), fikiria kutua video katika sehemu mbalimbali ili kutafakari au kujadili baadhi ya maswali yaliyopendekezwa katika shughuli hii.

  • Ni kwa jinsi gani adui anajaribu kukuongoza kwenye njia za dhambi? Ni chaguzi zipi ungeweza kufanya ili kubaki usalama kiroho?

  • Tazama majibu ya Daudi kwa hadithi ya Nathani katika 2 Samweli 12:1–6. Je, majibu yake yanapendekeza nini kuhusu jinsi Daudi alivyojiona mwenyewe? Bwana amefanya nini ili kukusaidia kujiona wewe mwenyewe kwa usahihi zaidi?

  • Ni kwa jinsi gani ungeweza kufupisha matukio ya 2 Samweli 11–12 katika onyo la sentensi moja?

Kusoma kuhusu chaguzi mbaya za Daudi kunaweza kukuongoza kujifunza kuhusu hatari za ponografia na dhambi ya ngono. Nyenzo nzuri kwa ajili ya hili ni Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, hasa sehemu zenye kichwa cha habari “Nini cha kufanya kwa sasa” na “Mwili wako ni mtakatifu” (kurasa 21–28). Pengine ungeweza kuangalia katika nyenzo hiyo kwa ajili ya ushauri ambao ungemsaidia Daudi kufanya chaguzi nzuri zaidi. Au ungeweza kusoma “Yesu Kristo atakusaidia” (ukurasa wa 6–9), ukitafuta kitu ambacho kingemsaidia Daudi kurudi kwa Bwana.

Fikiria kuimba wimbo kama “Ninakuhitaji” (Nyimbo za Dini, na. 47) na kutafakari jinsi Mwokozi alivyokuimarisha wakati ulipokabiliwa na majaribu.

Ona pia 2 Nefi 28:20–24; Ulisses Soares, “Mtafuteni Kristo katika Kila Wazo,” Liahona, Nov. 2020, 82–85; “Kuchukua Jukumu la Teknolojia,” Maktaba ya Injili; “Watch Your Step” (video), Maktaba ya Injili.

2:36

Watch Your Step

1 Wafalme 3:1–15

Kipawa cha utambuzi kinanisaidia mimi kutofautisha mema na mabaya.

Ikiwa Bwana atakwambia, “Omba utakalo nikupe” (1 Wafalme 3:5), ni nini ungeomba? Ni nini kinachokuvutia kuhusu ombi la Sulemani? Tafakari kwa nini, “moyo wa adili” “kupambanua kati ya mema na mabaya” (mstari 9) ni kipawa cha thamani. Je, unaweza kufanya nini ili kutafuta kipawa hiki?

Ona pia Moroni 7:12–19.

1 Wafalme 6–8; 9:1–9

Kupitia maagano yaliyofanywa katika nyumba ya Bwana, Bwana hukaa nami.

Katika 1 Wafalme 6–7 utapata maelezo ya kina ya nyumba takatifu ambayo Sulemani aliijenga kwa ajili ya Bwana. Utondoti unaweza usionekane kuwa muhimu kwako kama ilivyokuwa kwa Waisraeli wa kale. Lakini kusoma sura hizi kunaweza kukupa hisia ya jinsi ilivyokuwa muhimu kwao kuwa na nyumba ya Bwana. Kwa nini ni muhimu kwako?

Unaweza kutafakari ni sehemu gani tofauti za hekalu la Sulemani zinaweza kuashiria. Kwa mfano, fikiria kile kerubi, miti, na maua katika 1 Wafalme 6:35 vinaweza kuwakilisha nini. (Ona pia Musa 3:24.)

Sura ya 8 imeandikwa sala ya Sulemani baada ya kukamilisha hekalu (ona mstari wa 22–61). Fikiria kutengeneza orodha ya baraka Sulemani alizoomba. Kitu gani kinakuvutia kuhusu baraka hizi? (Tazama pia ahadi za Bwana katika 1 Wafalme 6:11–13; 9:1–9.) Kama umepata kuwa kwenye nyumba ya Bwana, fikiria kuhusu uzoefu wako wa kuabudu huko. Ni kwa jinsi gani kushika maagano ya hekaluni kumekusaidia kupata baraka za Bwana?

Ona pia Mafundisho na Maagano 109; Henry B. Eyring, “Ninapenda Kuona Hekalu,” Liahona, Mei 2021, 28–31.

Hekalu la Barranquilla Colombia

Hekalu la Barranquilla Colombia

1 Wafalme 8:61; 11:1–11

“Moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana.”

Inamaanisha nini “ mioyo [yetu] na … iwe mikamilifu kwa Bwana”? (1 Wafalme 8:61). Je, hiyo ni tofauti na matendo yetu kuwa makamilifu? Kwa jinsi gani? Soma 1 Wafalme 11:1–11, na utambue kile Bwana alisema kuhusu moyo wa Sulemani. Unaweza kutafakari kama kuna ushawishi katika maisha yako ambao unaweza kugeuza moyo wako mbali na Bwana na kuelekea “miungu mingine.”

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

2 Samweli 11

Bwana anaweza kunibariki ninapokuwa najaribiwa.

  • Mfalme Daudi” katika Hadithi za Agano la Kale, 117–20, inaweza kukusaidia kuwaambia watoto wako hadithi katika 2 Samweli 11. Unaweza kuwaomba watoto wako watambue chaguzi mbaya Daudi alizofanya na kupendekeza chaguzi nzuri ambazo angeweza kufanya badala yake. Ni nini baadhi ya vitu tunavyoweza kufanya tunapokuwa tunajaribiwa ambavyo vinaweza kutusaidia kufanya chaguzi sahihi?

    2:11

    King David

  • Kusoma kuhusu dhambi za majonzi za Daudi kunaweza kuwa nafasi nzuri ya kujadili hatari za picha za ponografia, . Video, “What Should I Do When I See Pornography?” (Maktaba ya Injili) ina mwongozo wenye msaada. Wasaidie watoto wako kutengeneza mpango kuhusu nini wataweza kufanya wakati wanapokabiliana na ponografia.

    5:46

    What should I do when I see pornography?

1 Wafalme 8:22–61

Kufanya maagano katika nyumba ya Bwana—na kuyashika—hunisaidia kutembea katika njia Zake.

  • Wakati wewe na watoto wako mnapojifunza kuhusu kuwekwa wakfu kwa hekalu katika 1 Wafalme 8, mnaweza kuangalia picha za mahekalu katika muhtasari wa wiki hii. Waache watoto wako wazungumze kuhusu kile wanachoona katika picha. Unaweza kusisitiza mstari wa 57–58. Ina maana gani “kutembea katika njia zote za [Bwana]”? (1 Wafalme 8:58). Pengine watoto wako wangeweza kuchukua hatua kwa kila jibu wanalotoa.

  • Waambie watoto wako jinsi kushika maagano unayofanya hekaluni kunakusaidia wewe kutembea katika njia za Bwana. Unaweza kuwaambia maagano haya ni nini (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 27.2, Maktaba ya Injili). Mngeweza pia kuimba wimbo pamoja kama: “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95).

Hekalu la Sulemani

Kielelezo cha hekalu la Sulemani, na Sam Lawlor

1 Wafalme 11:1–11

Ninaweza kumweka Bwana kuwa wa kwanza katika maisha yangu.

  • Kusoma kuhusu jinsi wake za Sulemani walivyomshawishi kungeweza kuongoza kwenye mazungumzo kuhusu mifano ya “miungu wengine”—au vitu ambavyo watu wanaviabudu au kuvipenda badala ya Bwana. Ni kwa jinsi gani tunaonyesha kwamba tunampenda Yeye zaidi ya kitu kingine cho chote katika maisha yetu?

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Hekalu la Sulemani

Kuwekwa Wakfu kwa Hekalu la Sulemani katika Yerusalemu, na William Hole

Ukurasa wa shughuli ya Msingi: Kufanya maagano katika nyumba ya Bwana kunanisaidia kutembea katika njia Zake