“Juni 1–7. ‘Moyo Wangu Wamshangilia Bwana’: Ruthu 1; 1 Samweli 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Juni 1–7. ‘Moyo Wangu Wamshangilia Bwana,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Popote Uendapo, by Sandy Freckleton Gagon
June 1-7: “Moyo Wangu Wamshangailia Bwana,”
Ruthu; 1 Samweli 1–7
Wakati mwingine tunafikiri kwamba maisha yetu yanapaswa yafuate njia iliyo wazi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Umbali mfupi zaidi kati ya nukta mbili ni mstari ulionyooka, baada ya yote. Na bado maisha mara nyingi yamejaa kuchelewa kwingi na michepuko ambayo hutupeleka katika mwelekeo tusiotarajia.
Ruthu na Hana hakika walilijua hili. Ruthu hakuwa Mwisraeli, ila aliolewa na mmoja wao, na wakati mume wake alpofariki, alikuwa na uchaguzi wa kufanya. Je, angerudi kwenye familia yake na maisha yake ya awali, maisha aliyoyazoea au angekumbatia imani ya Waisraeli na nyumba mpya pamoja na mama mkwe wake? (ona Ruthu 1:4–18). Mpango wa Hana wa maisha yake ulikuwa ni kuzaa watoto, lakini hakuweza kufanya hivyo na hilo lilimwacha yeye “katika maumivu ya moyo” (ona 1 Samweli 1:1–10). Unaposoma kuhusu Ruthu na Hana, fikiria imani wanayoweza kuwa walikuwa nayo kusafiri katika njia zao wasizotarajia. Kisha fikiria kuhusu safari yako mwenyewe. Ni tofauti na ya Ruthu na ya Hana—na mwingine ye yote yule. Lakini kipindi chote cha majaribu na mshangao kati ya hapa na mwisho wa safari yako ya milele, unaweza kujifunza kusema pamoja na Hana, “Moyo Wangu Wamshangilia Bwana” (1 Samweli 2:1).
Ona pia Kamusi ya Biblia kwa ajili ya muhtasari wa vitabu vya Ruthu na 1 Samweli.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ruthu
Yesu Kristo anaweza kugeuza majanga kuwa ushindi.
Maisha ni magumu kwa mjane katika zama zo zote. Lakini wakati mume wa Ruthu alipofariki, hali yake ilikuwa na ugumu hasa. Katika utamaduni wa Kiisraeli wakati huo, mwanamke asiye na mume au watoto hawakuwa na haki ya kumiliki mali na walikuwa na njia chache za kujipatia kipato. Unaposoma hadithi ya Ruthu, gundua jinsi Bwana alivyobadili majanga kuwa baraka kuu. Unagundua nini kuhusu Ruthu ambacho kingeweza kumsaidia? Ni kwa jinsi gani Boazi alimkomboa Ruthu kutokana na hali yake ya kukata tamaa? (ona Ruthu 4:4–10). Ni kwa jinsi gani Ruthu na Boazi walikuwa kama Yesu Kristo?
Ona pia ““Be Still, My Soul,” Nyimbo za Dini, no. 124.
Ruthu; 1 Samweli 1
Ninaweza kuamini kwamba Mungu anaweza kunilinda na kunisaidia bila kujali hali yangu.
Labda umeumia sana kwa kupoteza mengi, kama Ruthu na Naomi walivyokuwa (ona Ruthu 1:1–5). Au pengine, kama Hana, unatamani baraka ambazo bado hujapokea (ona 1 Samweli 1:1–10). Ni kwa jinsi gani wanawake hawa walionyesha imani yao kwa Mungu? Je, unajifunza nini kutokana na mifano yao?
Bila shaka, sio kila mtu anaye sali kwa ajili ya kupata mtoto humpokea mmoja, na sio kila mtu ambaye mwenzi wake anakufa anaolewa au anaoa tena. Lakini kila mtu anayemgeukia Mwokozi anapokea usaidizi na mwongozo Wake. Fikiria jinsi ambavyo “umekuja kumwamini” Bwana (Ruthu 2:12) katika wakati mgumu wa maisha yako.
Ona pia Amy A. Wright, “Kaeni Siku katika Kristo,” Liahona, Nov. 2023, 9–11.
Kwa Ajili ya Mtoto Huyu Niliomba, na Elspeth Young
1 Samweli 2; 1–7
Ili kupokea msaada wa Bwana, ninahitaji kumwamini Yeye na kutii amri Zake.
Wakati maadui zao waliposhambulia, Waisraeli inaonekana walifikiri kwamba kumiliki tu sanduku la agano kungewalinda. Unaposoma 1 Samweli 4–6, fikiria kuhusu kwa nini hilo halikufanya kazi. (Tazama pia matendo yasiyo ya haki ya wana wa Eli, ambao walihudumu kama makuhani katika tabernakulo, katika 1 Samweli 2:12–25.) Je, unafikiri ni nini Bwana alikuwa anajaribu kuwafundisha watu Wake? Unajifunza nini kutokana na kile kilichotokea kwa Wafilisti baada ya kuteka sanduku? (ona sura ya 5–6). Unajifunza nini kutokana na juhudi za Israeli za kupata tena ulinzi wa Bwana katika 1 Samweli 7?
Unaweza kuvutiwa kwa kusoma shairi la Hana la sifa katika 1 Samweli 2:1–10. Unapata nini katika maneno yake ambacho kingeweza kuwasaidia wana wa Eli na Waisraeli wengine waliosalia?
1 Samweli 3
Ninaweza kusikia na kutii sauti ya Bwana.
Nyakati zingine, unaweza kuhisi kama Samweli, ambaye alisikia sauti ya Bwana lakini hakuitambua. Kama sisi sote, Samweli alipaswa kujifunza namna ya kutambua sauti ya Bwana. Wakati unapojifunza 1 Samweli 3, unajifunza nini kutoka kwa mvulana huyu mdogo kuhusu kusikia na kutii sauti ya Bwana? Unaweza pia kupekua maandiko haya ya ziada na kutengeneza orodha ya miongozo ambayo inaweza kumsaidia mtu kutambua sauti ya Bwana: 1 Wafalme 19:11–12; Luka 24:15–32; 3 Nefi 11:3–7; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:7–9.
Nyakati zingine, unaweza kuhisi kwamba mbingu zimefungwa na kwamba Mungu hataki kuwasiliana nawe. Rais Russell M. Nelson alisema: “Je, Mungu kweli anataka kuzungumza na wewe? “Ndiyo!” (“Ufunuo kwa Kanisa, Ufunuo kwa ajili Ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 93–96. Unapojifunza ujumbe wa Rais Nelson, unapata nini ambacho kinakutia msukumo wa kusikia na kutii sauti ya Bwana? Rais Nelson anakualika ufanye nini, na ni baraka gani anazoahidi? Unaweza pia kupata mialiko na baraka zilizoahidiwa kuhusu ufunuo katika “Enenda katika Nuru ya Mungu” (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 16–20). Fikiria kuchagua kitu kimoja unachoweza kufanya ili “kuongeza uwezo wako wa kiroho wa kupokea ufunuo.”
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ruthu
Ninaweza kuonyesha upendo na ukarimu kwa watu wanaonizunguka.
-
Unaposhiriki na watoto wako hadithi ya Ruthu (ungeweza kutumia “Ruthu na Naomi” katika Hadithi za Agano la Kale, 100–103), waalike kuinua mikono yao kila mara wanaposikia tendo la ukarimu katika hadithi. Wangeweza pia kushiriki jinsi wanavyohisi wakati wengine wanapokuwa wakarimu kwao, au wanapokuwa wakarimu kwa wengine. Ni kwa jinsi gani Mwokozi amekuwa mkarimu kwetu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano Wake? (ona “Kindness Begins with Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145).
2:0Ruth and Naomi
Ruthu; 1 Samweli 1
Ninaweza kuwa na imani katika Bwana.
-
Hadithi za Ruthu na Hana zinaweza kuwavutia watoto wako wabaki waaminifu katika nyakati ngumu. Fikiria kuwasaidia kutengeneza chati rahisi yenye vichwa vya habari Majaribu, Matendo, Baraka. Kisha ungeweza kusoma pamoja nao Ruthu 1:3–5, 8, 16; 2:1–3, 8–12; 4:13–17; 1 Samueli 1:1–18 na waandike chini ya vichwa hivyo kile wanachopata kwenye mistari hii. Ruthu na Hana wanaonyeshaje imani yao katika Bwana? Wewe au watoto wako mngeweza kisha kushiriki mifano ya jinsi Bwana alivyowabariki wakati wa nyakati ngumu.
1 Samweli 1:1–18
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu maombi yangu.
-
Ili Kujifunza kuhusu Hana, watoto wako wangeweza kusoma 1 Samweli 1:1–18 au “Hana” katika Hadithi za Agano la Kale (104–5) au kutazama “Hannah’s Faith” (video, Maktaba ya Injili). Inaweza kuwa ya kufurahisha kurusha mpira kwa mtoto na kuwaalika wasimulie sehemu ya hadithi kabla ya kupitisha mpira kwa mtu mwingine. Tunajifunza nini kuhusu sala kutokana na mfano wa Hana?
1:15Hannah
3:9Hannah's Faith
Samuel Anamwambia Eli Ukweli, na Robert T. Barrett
1 Samweli 3:1–10
Ninaweza kusikia na kutii sauti ya Bwana.
-
Pengine igizo rahisi la kuigiza lingeweza kuwasaidia watoto wako wajifunze kutokana na uzoefu wa Samweli na ufunuo. Mtoto mmoja angeweza kujifanya kuwa Samweli, na mwingine angeweza kujifanya kuwa Eli unaposoma 1 Samweli 3:1–10 (ona pia “Samweli Nabii” katika Hadithi za Agano la Kale, 106–9, au video “Samuel and Eli,” Maktaba ya Injili). Tunajifunza nini kutoka kwa Samweli kuhusu jinsi ya kusikia sauti ya Bwana? Je, ni kwa jinsi gani tunaonyesha kwamba tuko radhi kumsikia Bwana anaposema nasi?
2:10Samuel the Prophet
1:58Samuel and Eli
-
Waulize watoto wako jinsi ambavyo wangemwelezea mtu jinsi Bwana anavyosema nao. Ungeweza kuwasaidia kutafuta majibu katika Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:7–9.
Wasaidie watoto wako wajifunze kumtambua Roho. Si rahisi kutambua kati ya hisia zetu wenyewe na Roho Mtakatifu. Kila mtu anahangaika na hili mara kwa mara. Chukua kila fursa unayoweza kuwasaidia watoto wako watambue wakati wanapohisi ushawishi wa Roho. Kwa mfano, unaposoma 1 Samweli 3:1–10 na mistari iliyopendekezwa katika Mafundisho na Maagano, ungeweza kushiriki uzoefu ambapo Bwana amekufundisha katika akili yako na moyo wako.
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .