Njoo, Unifuate
Juni 15–21. “Vita ni vya Bwana”: 1 Samweli 17–18; 24–26; 2 Samweli 5–7


“Juni 15–21. ‘Vita ni vya Bwana’: 1 Samweli 17–18; 24–26; 2 Samweli 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Juni 15–21. ‘Vita ni vya Bwana,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Daudi ameshikilia kombeo

Daudi na Goliathi, na Steve Nethercott

Juni 15–21: “Vita ni vya Bwana”

1 Samueli 17–18; 24–26; 2 Samueli 5–7

Tangu makabila ya Israeli yalipofanya makazi katika nchi ya ahadi, Wafilisi wamekuwa tishio endelevu kwa usalama wao. Bwana alikuwa amewaokoa mara nyingi huko nyuma, lakini sasa wazee wa Israeli walidai, “Tunataka kuwa na mfalme … [ili] atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu” (1 Samweli 8:19–20). Kwa hivyo Sauli alipakwa mafuta kuwa mfalme. Na bado wakati tishio la jitu kubwa Goliathi alipotupa changamoto zake kwa majeshi ya Waisraeli, Sauli—kama wengine kwenye jeshi lake—“aliogopa sana” (1 Samweli 17:11). Katika siku ile, haikuwa Mfalme Sauli aliyewaokoa Waisraeli, bali kijana mnyenyekevu mchungaji wa kondoo aliyeitwa Daudi, ambaye hakuvaa deraya lakini alikuwa amevaa imani isiyopenyeka katika Bwana. Mapigano haya yalithibitisha kwa Israeli, na kwa ye yote ambaye ana vita ya kupigana vya kiroho, kwamba “Bwana haokoi kwa upanga na mkuki” na kwamba “vita ni vya Bwana” (1 Samweli 17:47).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

1 Samweli 17

ikoni ya seminari
Kwa msaada wa Bwana, ninaweza kushinda changamoto yo yote.

Hadithi ya Daudi na Goliathi ni mojawapo ya hadithi zinazojulikana sana katika maandiko. Bila shaka, kwa kawaida tunafokasi kwa Daudi. Lakini muda huu, unapojifunza 1 Samweli 17, tafakari pia maneno ya watu wengine katika sura hii (ona orodha hapo chini) Je, unajifunza nini kuhusu wao na nia zao? Je, unajifunza nini kuhusu Daudi? ni kwa jinsi gani yeye ni tofauti?

  • Goliathi: mstari wa 8–10, 43–44

  • Eliabu: mstari wa 28

  • Sauli: mstari wa 33

  • Daudi: mstari wa 26, 32, 34–37, 39, 45–47

Hadithi yako, ingawa haijulikani vizuri kama ya Daudi, ni hakika kujumuisha changamoto za ukubwa wa Goliathi ili kushinda na fursa za kutumia imani katika Bwana. Mfano wa Daudi unakufundisha nini kuhusu kukabiliana na dhiki katika hadithi yako? Unaweza pia kusoma ujumbe wa Rais Camille N. Johnson “Mwalike Kristo Aandike Hadithi Yako” (Liahona, Nov. 2021, 80–82) ukiwa na mojawapo ya changamoto zako akilini. Tafuta majibu kwa maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani Bwana ananitaka nizitazame changamoto zangu? Ni kwa jinsi gani Yeye amenisaidia katika siku zilizopita? Ni kwa jinsi gani ninaweza kuonyesha kwamba ninamwamini Yeye kuandika hadithi yangu?

Unaweza kuwa tayari unajua kwamba kuna baadhi ya sura za kutisha baadaye katika hadithi ya Daudi (ona, kwa mfano, 2 Samweli 11). Kama ungekuwa na nafasi ya kumpa Daudi baadhi ya ushauri baada ya vita vyake na Goliathi, ungesema nini? Ni kwa jinsi gani ahadi hii ingeweza kutumika kwenye maisha yako?

Ona pia “The Lord Will Deliver Me” (video), Gospel Library.

3:24

The Lord Will Deliver Me

1 Samweli 17:2650

Mtu mmoja mwenye imani katika Kristo anaweza kuleta tofauti.

Kwa nyongeza kwenye changamoto binafsi, sisi pia tunakumbana na matatizo makubwa, magumu ambayo yanaathiri ulimwengu wote. Wakati nguvu za uovu “zinakusanywa pamoja … kupigana” dhidi ya nguvu za wema (1 Samweli 17:1), tunaweza kujiuliza ni kwa jinsi gani juhudi zetu binafsi zinaweza kuleta tofauti. Je, unapata nini katika hadithi ya Daudi ambacho kinakupa tumaini?

Ona pia “Let Us All Press On,” Nyimbo za Dini, na. 243

Yonathani na Daudi

Urafiki wa Kweli na Kujiheshimu, na Wilson Ong (utondoti)

1 Samweli 18

“Yonathani alimpenda [Daudi] kama nafsi yake mwenyewe.”

Unaposoma 1 Samweli 18, fikiria kutofautisha Sauli na mwanawe Yonathani (ambaye, kama siyo kuwepo kwa Daudi, angedhania kuwa angekuwa mfalme anayefuata). Sauli na Yonathani waliitikia vipi mafanikio ya Daudi? Je, unaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu huu?

Unapata nini katika mitazamo na matendo ya Yonathani ambacho kinakukumbusha juu ya Yesu Kristo?

“Linganisha maandiko” (1 Nefi 19:23). Maandiko yanatoa fursa kubwa ya kujifunza kutokana na motisha na matendo ya watu kama Daudi, Yonathani, na Sauli. Utagundua kwamba hakuna ye yote katika maandiko asiye na dosari. Kwa hivyo unaposoma, kwa mfano, kuhusu chaguzi za uaminifu za Daudi, kuwa wazi kujifunza pia kutokana na makosa yake. Kufanya hivyo kunaweza kutusaidia kutambua uwezekano wa udhaifu ndani yetu na “kujifunza kuwa wenye busara zaidi ya [wengine] walivyokuwa” (Mormoni 9:31).

1 Samweli 24–26.

Msamaha ni njia ya uhakika kwenda kwenye amani na uponyaji.

Katika 1 Samweli 24–26, tafuta masomo kuhusu kiburi, msamaha, na udhibiti wa kibinafsi. Unaweza pia kufikiria kusoma ujumbe wa Mzee Mark A. Bragg “Utulivu-Kama-Kristo” kama sehemu ya kujifunza kwako (Liahona, Mei 2023, 60–63). Ni kwa jinsi gani Daudi, Abigaili, na wengine walionyesha—au kushindwa kuonyesha—utulivu kama wa Kristo katika sura hizi? Ni fursa gani ulizo nazo za kuonesha utulivu kama wa Kristoi?

Ujumbe wa Dada Kristen Yee “Taji la Maua Badala ya Majivu: Njia ya Uponyaji ya Msamaha” (Liahona, Nov. 2022, 36–39) unaweza kukusaidia kujifunza 1 Samweli 25. Ni kwa jinsi gani Abigal ni kama Yesu Kristo?

2 Samweli 5:17–25

Bwana anaweza kunipa mimi mwelekeo.

Hata baada ya Daudi kumshinda Goliathi, matatizo yake na Wafilisti hayakuisha. Unaposoma 2 Samweli 5:17–25, fikiria jinsi mfano wa Daudi unavyoweza kukusaidia wewe katika changamoto unazokabiliana nazo (ona pia 1 Samweli 23:2, 10–11; 30:8; 2 Samweli 2:1). Ni kwa jinsi gani unabarikiwa kwa kutenda kufuatana na ufunuo unaopokea?

2 Samweli 7

Ni “nyumba” gani Bwana alimuahidi Daudi?

Wakati Daudi alipojitoa kujenga nyumba, kumaanisha hekalu, kwa ajili ya Bwana (ona 2 Samweli 7:1–3), Bwana aliitikia kwamba mwana wa Daudi angeijenga (ona mstari wa 12–15; ona pia 1 Mambo ya Nyakati 17:1–15). Bwana pia alisema kwamba Yeye badala yake angemjengea Daudi “nyumba,” akimaanisha uzao, na kwamba kiti chake cha enzi kitadumu milele (ona 2 Samweli 7:11, 16, 25–29; Zaburi 89:3–4, 35–37). Ahadi hii ilitimizwa katika Yesu Kristo, Mfalme wetu wa Milele, ambaye alikuwa ni wa uzao wa Daudi (ona Mathayo 1:1; Luka 1:32–33; Yohana 18:33–37).

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

1 Samweli 17:20–54

Imani katika Yesu Kristo inaweza kunisaidia kuwa na ujasiri.

  • Unaweza kutaka kutumia “Daudi na Goliathi” katika Hadithi za Agano la Kale, 112–16, ili kuwasaidia watoto wako wajifahamishe na kile kilichotokea katika 1 Samweli 17:20–54. Kisha ungeweza kuwaacha wasimulie tena hadithi kwa kutumia picha au michoro ya mstari katika muhtasari huu. Waulize kile wanachofikiri Bwana anataka wajifunze kutoka kwenye hadithi hii.

    2:36

    David and Goliath

  • Wewe na watoto wako mngeweza pia kutengeneza orodha ya baadhi ya changamoto ngumu wanazoweza kukabiliana nazo wakati wa maisha yao. Kisha wasaidie kutafuta vitu ambavyo Daudi alisema ambavyo vinaweza kusaidia katika changamoto hizi (ona 1 Samweli 17:26, 32, 34–37, 45–47). Waambie watoto jinsi Yesu Kristo alivyokusaidia wewe wakati wa changamoto.

  • Watoto wako wangeweza kutembea kama vile wao ni Daudi akienda kupigana na Goliathi huku wakiimba wimbo kuhusu kuwa na ujasiri, kama vile “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162).

1 Samweli 18:1–4

Marafiki wazuri wanaweza kuwa baraka kutoka kwa Mungu

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto wako wajifunze kutokana na urafiki wa Yonathani na Daudi? Njia moja ingekuwa ni kumpa kila mtoto karatasi, mbili zenye umbo la moyo, moja kumwakilisha Daudi na lingine kumwakilisha Yonathani. Kisha someni pamoja virai vichache kutoka 1 Samweli 18:1–4 ambavyo vinasisitiza upendo ambao hawa marafiki wawili walihisi kwa kila mmoja. Watoto wenu wangeweza kisha kuandika au kuchora kwenye mioyo yao ya karatasi jinsi wanavyoweza kuonyesha upendo kwa rafiki.

2 Samweli 5:19, 23

Kama ninahitaji mwongozo, ninaweza kumuomba Baba wa Mbinguni.

  • Katika sura hizi, Daudi alikuwa mfalme wa Israeli. Inaweza kuwa ya kufurahisha kwa watoto wako kujifanya kuwa mfalme au malkia. Ni sheria zipi wangengeneza? Watakwenda wapi kwa ajili ya msaada? Wasaidie watoto wako kugundua kwamba wakati Daudi alihitaji msaada, “aliuliza,” au aliomba, kwa ajili ya majibu. Kwa mfano unaposoma 2 Samweli 5:19, 23, waalike watoto wasikilize kwa ajili ya neno “aliuliza” na wakunje mikono yao wanapolisikia. Kwa nini Daudi alihitaji msaada wa Bwana katika jukumu lake jipya?

  • Ambianeni kila mmoja kuhusu wakati ambapo uliomba msaada kwa Baba wa Mbinguni. Ilileta tofauti gani kupata Yeye kukusaidia wewe?

msichana akisali

2 Samweli 7:16–17

Yesu Kristo ni Mfalme wangu wa Milele

  • Wafalme tunaosoma kuwahusu katika Agano la Kale wote walikuwa na dosari na Falme zao zote ziliisha. Lakini Yesu Kristo ni Mfalme mkamilifu na atatawala milele. Unaweza kuwasaidia watoto wako wagundue hili kwa kusoma pamoja kile nabii Nathani alimwambia Mfalme Daudi katika 2 Samweli 7:16–17. Ni kwa jinsi gani ufalme wa Daudi haungekuwa na mwisho? Wasaidie watoto wako kutafuta na kusoma vifungu vya maandiko ambavyo vinafundisha kwamba Yesu Kristo, wa ukoo wa Daudi, ni Mfalme wetu kama vile Luka 1:32–33; Yohana 18:33–37; na Ufunuo 19:16. Ni kwa jinsi gani Yesu ni tofauti na wafalme wa duniani? Ni kwa jinsi gani tunamheshimu Yesu Kristo kama Mfalme wetu wa Milele?

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Daudi na Goliathi

Kielelezo cha Daudi, na Dilleen Marsh

ukurasa wa shughuli za Msingi: Imani katika Yesu Kristo inaweza kutusaidia kuwa na ujasiri