Njoo, Unifuate
Mawazo ya Kuweka Akilini: “Yesu Atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani’”


“Mawazo ya Kuweka Akilini: ‘Yesu Atasema kwa Israeli Yote, “Njooni Nyumbani”’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2026 (2026)

“Mawazo ya kuweka akilini: ‘Yesu Atasema kwa Israeli Wote, “Njooni Nyumbani,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

“Yesu Atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani’”

Katika jangwa la Sinai, Musa aliwakusanya wana wa Israeli chini ya mlima. Pale Bwana alitangaza kwamba Yeye alitaka kugeuza kundi hili la watumwa waliokombolewa karibuni kuwa watu imara. “Mtakuwa kwangu,” Alisema, “ufalme wa makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:6). Aliahidi kwamba watastawi na kufanikiwa, hata kama watakuwa wamezungukwa na kundi kubwa na lenye nguvu la maadui..

Haya yote yangetokea sio kwa sababu Waisraeli walikuwa wengi au wenye nguvu au wenye ujuzi. Yangetokea, Bwana alielezea, kama kweli “wangetii sauti [Yake], na kulishika agano [Lake]” (Kutoka 19:5). Ni nguvu za Mungu, na sio zao wenyewe, ambazo zingewafanya wao kuwa imara.

Na bado Waisraeli siyo daima walitii sauti ya Mungu, na baada ya muda waliacha kushika agano Lake. Wengi waliabudu miungu wengine na kurithi mapokeo ya tamaduni zilizowazunguka. Walikataa kitu kile hasa kilichowafanya wao kuwa taifa tofauti—uhusiano wao wa agano na Bwana. Pasipokuwa nguvu za Mungu za kuwalinda wao, hapakuwa na cho chote cha kuwazuia maadui zao.

Kutawanyika

Mara kadhaa kati ya 735 na 720 KK, Waashuru walivamia Ufalme wa Kaskazini wa Israeli, nyumbani kwa makabila kumi kati ya kumi na mawili, na kuwachukua mateka maelfu ya Waisraeli mateka na kuwapeleka sehemu mbalimbali za Himaya ya Ashuru. Waisraeli hawa walikuja kujulikana kama “makabila yaliyopotea,” kwa sehemu ni kwa sababu walikuwa wametolewa kutoka katika nchi yao na kutawanywa miongoni mwa mataifa mengine. Lakini walikuwa pia wamepotea katika ufahamu mpana: kwa muda walipoteza hisia za ufahamu wa utambulisho wao kama watu wa agano wa Mungu.

Hatimaye watu wengi katika Ufalme wa Kusini wa Yuda pia waligeukia mbali kutoka kwa Bwana. Waashuru walishambulia na kuteka sehemu kubwa ya ufalme huo pia; Yerusalemu pekee ndiyo iliyohifadhiwa kimiujiza. Baadaye, kati ya mwaka 597 na 580 KK, Wababeli waliiharibu Yerusalemu, ikijumuisha hekalu, na kuwachukua watu wengi mateka. Karibia miaka 70 baadaye, masazo ya Yuda yaliruhusiwa kurudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu. Wengi, hata hivyo, walibaki Babeli.

Yerusalemu iliteketezwa kwa moto

Kuangamizwa kwa Yerusalemu na Nebuzari-adani,, na William Brassey Hole, © Providence Collection/licensed from goodsalt.com

Kadiri muda ulivyopita, Waisraeli kutoka makabila yote “walitawanywa … kwa upepo wa kisulisuli, miongoni mwa mataifa yote wasiowajua.” (Zakaria 7:14) . Baadhi Bwana aliwaongoza mbali kwenye nchi zingine. Wengine waliondoka Israeli ili kutoroka kukamatwa au kwa sababu za kisiasa au za kiuchumi.

Tunaita matukio yote haya ni kutawanywa kwa Israeli. Na ni muhimu kujua kuhusu kutawanywa kwa sababu kadhaa. Kwa sababu moja, ni mada kuu ya Agano la Kale: manabii wengi wa Agano la Kale walikuwa ni mashahidi wa kudorora kiroho ambako kulisababisha kutawanywa. Manabii hao waliona kabla na kuonya kuhusu hilo. Baadhi yao hata waliishi kupitia hilo. Hiyo inasaidia kukumbuka wakati unaposoma vitabu vya Isaya, Yeremia, Amosi, na manabii wengine katika sehemu ya mwisho ya Agano la Kale. Pamoja na muktadha huu akilini, unaposoma unabii wao kuhusu Ashuru na Babeli, kuabudu sanamu na utumwa, uharibifu na hatimaye urejesho, utajua nini wanachokiongelea.

Kuelewa kutawanywa kwa Israeli kutakusaidia wewe kuelewa kitabu cha Mormoni vizuri zaidi pia, kwa sababu Kitabu cha Mormoni ni kumbukumbu ya tawi la Israeli iliyotawanywa. Kumbukumbu hii inaanza na familia ya Lehi wakitoroka Yerusalemu mnamo 600 KK, kabla ya uvamizi wa Wababeli. Lehi alikuwa mmojawapo wa manabii hao waliotoa unabii wa kutawanywa kwa Israeli. Na familia yake ilisaidia kutimiza unabii huo, wakichukua tawi lao la nyumba ya Israeli na kulipanda katika upande mwingine wa dunia, katika mabara ya Amerika.

Kusanyiko

Kutawanyika kwa Israeli, hata hivyo, ni nusu tu ya hadithi. Bwana hasahau watu Wake, wala hawatelekezi, hata wakati wao ndio wamemwacha Yeye. Unabii mwingi kwamba Mungu angewatawanya Israeli uliendana na ahadi nyingi kwamba siku moja angewakusanya tena.

Siku hiyo ni leo—siku yetu. Kukusanywa huko tayari kumeanza. Katika mwaka 1836, maelfu ya miaka baada ya Musa kuwakusanya wana wa Israeli chini ya Mlima Sinai, Musa alitokea katika Hekalu la Kirtland kumkabidhi Joseph Smith “funguo za kukusanyika kwa Israeli kutoka pande nne za dunia” (Mafundisho na Maagano 110:11). Sasa, chini ya uelekezi wa wale wanaoshikilia funguo hizi, makabila ya Israeli yanakusanywa kutoka kila taifa ambako watumishi wa Bwana wanaweza kwenda.

Musa akiwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland

Musa; Elia, na Eliya Wanatokea ndani ya Hekalu la Kirtland, na Gary E. Smith

Rais Russell M. Nelson ameliita kusanyiko hili “jambo muhimu sana linalofanyika duniani leo. Hakuna kingine kinafanana katika ukubwa, hakuna kingine kinachofanana nacho katika umuhimu, hakuna kingine kinachofanana nacho katika utukufu. Na kama utachagua, kama unataka, unaweza kuwa sehemu kubwa ya hilo.”

Je, ni kwa insi gani tunaweza kusaidia? Inamaanisha nini kuikusanya Israeli? Je, inamaanisha kurejesha makabila yale kumi na mawili katika nchi ambayo hapo mwanzo waliishi? Kimsingi, inamaanisha kitu kikubwa zaidi, cha milele zaidi. Kama vile Rais Nelson alivyofafanua:

“Tunapozungumza kuhusu kukusanywa, kiurahisi tunasema kanuni hii ya kweli: kila mmoja wa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni, katika pande zote mbili za pazia, anastahili kusikia ujumbe wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. …

Wakati wowote unapofanya kitu chochote kinachomsaidia mtu yeyote—upande wo wote wa pazia—kuchukua hatua moja mbele kufanya maagano na Mungu na kupokea ibada zao muhimu za ubatizo na za hekaluni, wewe unasaidia katika kukusanya Israeli. Ni rahisi tu kama hivyo.”

Hii inatokea, kama Isaya alivyosema, “mmoja mmoja” (Isaya 27:12) au, kama Yeremia alivyotabiri, “mtu mmoja wa mji mmoja,, na wawili wa jamaa moja” (Yeremia 3:14).

Kukusanya Israeli inamaanisha kuwarudisha watoto wa Mungu Kwake. Inamaanisha kuwarejesha kwenye uhusiano wao wa agano na Yeye. Inamaanisha kuanzisha upya “taifa takatifu” Yeye alilopendekeza kulianzisha muda mrefu uliopita (Kutoka 19:6).

Njooni Nyumbani

Kama mmoja ambaye amefanya agano na Mungu, wewe ni sehemu ya nyumba ya Israeli. Umekusanywa, na wewe ni mkusanyaji. Hadithi ya karne nyingi ya watu wa agano inajenga kilele chake, na wewe ni mchezaji muhimu. Sasa ni muda ambao “Yesu atasema kwa Israeli Wote, ‘Njooni Nyumbani.’”

Huu ni ujumbe wa wakusanyaji: Njooni nyumbani kwenye agano. Njooni Nyumbani Sayuni. Njooni nyumbani kwa Yesu Kristo, Mtakatifu wa Israeli, na Yeye atawaleta nyumbani kwa Mungu, Baba yenu.

Muhtasari

  1. Ona Kumbukumbu la Torati 28:1–14.

  2. Ona 2 Wafalme 17:6–7; 2 Mambo ya Nyakati 36:12–20

  3. Ona 2 Wafalme 17:1–7. Makabila kumi yaliyochukuliwa mateka na Ashuru yalikuwa Reubeni, Simeoni, Isakari, Zabuloni, Dani, Naftali, Gadi, Asheri, Efraimu, na Manase. Kabila la Lawi lilitawanywa katika himaya za makabila mengine ili liweze kutekeleza majukumu yake ya kikuhani.

  4. Ona 2 Wafalme 19; Isaya 10:12–13.

  5. Ona 2 Wafalme 24–25; 2 Mambo ya Nyakati 36; Yeremia 39; 52.

  6. Ona Ezra 17; Nehemia 2.

  7. Ona 2 Nefi 1:1–5; 1:15–16.

  8. Ona 2 Wafalme 25:22–26; Yeremia 42:13–19; 43:1–7.

  9. Katika mwaka wa 70 BK, Yerusalemu na hekalu lake viliharibiwa tena, safari hii na Warumi, na Wayahudi waliobaki walitawanywa kote katika mataifa mengi.

  10. Ona Yeremia 29:18; Ezekieli 22:15; Hosea 9:17; Amosi 9:9; 1 Nefi 1:13.

  11. Ona 1 Nefi 15:12.

  12. Ona 1 Nefi 1:13, 18–20; 10:12–14.

  13. Ona Isaya 5:26; 27:12; 54; Yeremia 16:14–15; 29:14; 31:10; Ezekieli 11:17; 34:12; 37:21–28; Zakaria 10:8; 1 Nefi 10:14; 22:25; 3 Nefi 16:1–5; 17:4.

  14. Russell M. Nelson, “Hope of Israel” (worldwide youth devotional, June 3, 2018), Gospel Library.

  15. Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli.”

  16. Ona 2 Nefi 30:2.

  17. Tuishangilie Siku ya Wokovu,” Nyimbo za Dini, na. 3.