Njoo, Unifuate
Julai 6–12. “Yupo Nabii katika Israeli”: 2 Wafalme 2–7


“Julai 6–12. ‘Yupo Nabii katika Israeli’: 2 Wafalme 2–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Julai 6–12. ‘Yupo Nabii katika Israeli,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Naamani katika Mto Yordani

Katika Ukingo wa Mto, na Annie Henrie Nader

Julai 6–12: “Yupo Nabii katika Israeli”

2 Wafalme 2–7

Misheni kuu zaidi ya nabii ni kufundisha na kushuhudia juu ya Mwokozi Yesu Kristo. Kumbukumbu zetu juu ya nabii Elisha, hata hivyo, hazijumuishi mengi sana juu ya mafundisho yake au kushuhudia kwake. Kile ambacho kumbukumbu zinajumuisha ni miujiza Elisha aliyoifanya, ikijumuisha kumfufua mtoto kutoka katika wafu (ona 2 Wafalme 4:18–37), kulisha umati kwa kiasi kidogo cha chakula (ona 2 Wafalme 4:42–44), na kumponya mkoma (ona 2 Wafalme 5:1–14). Kwa hiyo wakati hatuna maneno ya Elisha kuhusu Kristo, tuna huduma na miujiza ya Elisha, ambayo inashuhudia juu ya Kristo. Ni madhihirisho yenye nguvu ya Bwana yenye kupatiana uhai , kurutubisha, na kuponya. Miujiza inatokea mara nyingi zaidi katika maisha yetu kuliko tunavyotambua. Ili kuiona, tunahitaji kutafuta imani aliyokuwa nayo Elisha wakati aliposali kwa niaba ya mtumishi wake kijana mwoga, “Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona” (2 Wafalme 6:17).

Kwa maelezo zaidi kuhusu 2 Wafalme, ona “Wafalme, vitabu vya” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

2 Wafalme 2–6

Mungu anaweza kutenda miujiza katika maisha yangu.

Miujiza hutuonyesha nguvu za Mungu. Inaweza kutusaidia kushinda yaliyo magumu ya maisha ya duniani—kama nchi kame ambayo inahitaji maji safi (ona 2 Wafalme 2:19–22) au shoka lililopotea ambalo linahitaji kupatikana tena (ona 2 Wafalme 6:4–7). Lakini muhimu zaidi, miujiza inaweza kutugeuza kwa Bwana. Unaposoma 2 Wafalme 2–6, fikiria kutengeneza orodha ya miujiza uliyopata, na utafakari masomo ya kiroho uliyojifunza kutoka kwa kila moja.

Mnaweza pia kulinganisha miujiza Elisha aliyofanya na miujiza ambayo Yesu Kristo alifanya (ona 2 Wafalme 4:8–37 na Luka 7:11–16; 2 Wafalme 4:42–44 na Yohana 6:1–13; 2 Wafalme 5:1–15 na Luka 17:11–19). Miujiza hii inakufundisha nini kuhusu Mwokozi na manabii Wake?

Ona pia 2 Nefi 26:12–13; 27:23; Moroni 7:35–37; sehemu “Tafuta na kutarajia miujiza” katika Russell M. Nelson, “Nguvu ya Kasi ya Kiroho,” Liahona, Mei 2022, 99–100.

Elisha akimrudishia uhai mtoto kutoka kwa wafu

Elisha Akimrudishia Uhai Mwana wa Mshunami, na Frederic Leighton

2 Wafalme 4:8–17; 7:1–16

Bwana atatimiza maneno Yake yaliyotolewa kupitia manabii Wake.

Bwana alimtia msukumo Elisha kutoa unabii juu ya vitu vitakavyokuja—kwa kawaida, vitu ambavyo vilionekana visingeweza kutokea. Unaposoma 2 Wafalme 4:8–17; 7:1–16, fikiria kuhusu jinsi unavyoitikia neno la Bwana kupitia manabii Wake leo. Ni mafundisho, unabii, au ahadi gani ulizozisikia kutoka kwa manabii walio hai? Je, unafanya nini ili kutenda katika imani juu ya maneno yao?

Ona pia 3 Nefi 29:6; Mafundisho na Maagano 1:37–38;Mkusanyiko wa “Teachings of Presidents”, Gospel Library.

2 Wafalme 5

Kwa vile mimi ni mnyenyekevu na mtiifu, Yesu Kristo anaweza kuniponya.

Unaposoma 2 Wafalme 5, fikiria kulinganisha ukoma wa Naamani na changamoto ya kiroho unayokabiliana nayo.

Je, kuna mtu kama “mjakazi mdogo” katika maisha yako, akikuhimiza kutafuta mwongozo kuhusu changamoto yako kutoka kwa manabii wa Bwana? (ona mstari wa 2–3, 13).

Je, Bwana anakualika kufanya nini ambacho kinaweza kuonekana rahisi sana—kama “kuosha, na kuwa msafi”? (mstari wa 13). Ni nini kinaweza kuwa kinakuzuia kukubali mialiko Yake rahisi?

Unawezaje kuonyesha unyenyekevu kama Naamani alivyofanya?

Angalia jinsi uzoefu wa Naamani ulivyoathiri imani yake katika Mungu wa Israeli (ona mstari wa 15). Unaweza kujifunza nini kutokana na hili?

Ona pia Luka 4:27; 1 Petro 5:5–7; Alma 37:3–7; Etheri 12:27; L. Whitney Clayton, “Lolote Yeye Akwambialo Wewe, Litende,” Liahona, Mei 2017, 97–99; “Naaman and Elisha” (video), Maktaba ya injili

14:30

Naaman and Elisha

Linganisha maandiko kwa maisha Yako. Wakati mwingine ni rahisi kutafuta maana binafsi katika maandiko wakati unapolinganisha vitu vya kimwili katika hadithi na vitu vya kiroho katika maisha yako Kwa mfano, unapojifunza 2 Wafalme 2–7, unaweza kulinganisha hali katika maisha yako na vitu kama ukoma, shoka lililoazimwa, Mto Yordani, au jeshi kubwa linalovamia. Ni masomo gani yawezekanaBwana anayo kwa ajili yako katika hadithi hizi?

2 Wafalme 6:8–23

ikoni ya seminari
“Walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”

Unapojaribu kumfuata Kristo, je, umewahi kuhisi kama mtumishi kijana wa Elisha—kuzidiwa kiasi kikubwa na mwenye kutishika? JIfanye kuwa ulikuwa mahali pake unaposoma 2 Wafalme 6:8–23. Ni kwa jinsi gani hadithi hii inabadilisha namna unavyofikiri na kuhisi kuhusu majaribu yako, wajibu wako, au juhudi zako za kuishi injili?

Wakati unapoafakari, fikiria maneno ya Rais Henry B. Eyring: “kama yule mtumishi wa Elisha, kuna wengi walio na wewe kuliko wale unaoweza kuwaona wakikupinga wewe. Baadhi ambao wako na wewe watakuwa hawaonekani kwa macho yako ya kimwili. Bwana atakuinua juu na nyakati zote atafanya hivyo kwa kuwaita wengine kusimama na wewe” (“O ye That Embark,” Liahona,, Nov. 2008, 58).

Fikiria kutengeneza orodha ya “wale walio pamoja [nawe]” (mstari wa 16)—watu ambao Mungu amewaweka katika maisha yako ili kukusaidia. Unaweza kumwomba Yeye akusaidie kuwatambua kwa kufungua macho yako ya kiroho. Pengine pia amekuweka wewe katika maisha ya wengine ili kuwasaidia. Ni kwa jinsi gani unaweza kupata nguvu na msaada kutoka kwa kila mmoja?

Ni lini umehisi msaada ambao Bwana anauelezea katika Mafundisho na Maagano 84:88?

Unaweza pia kujifunza ujumbe wa Dada Michelle D. Craig “Macho ya Kuona” (Liahona, Nov. 2020, 15–17). Jiulize, “Mungu anataka mimi nione nini?”

Kurejelea hadithi katika 2 Wafalme 6:8–23, Mzee Ronald A. Rasband alisema: “Tunaweza au tusiweze kuwa na magari ya moto yaliyotumwa kuondoa woga wetu na kushinda mapepo yetu, lakini somo ni wazi. Bwana yu pamoja nasi, anatujali na anatubariki katika njia ambazo ni Yeye pekee ndiye anayeweza kufanya hivyo. Sala inaweza kushusha chini nguvu na ufunuo ambao tunahitaji ili kulenga mawazo yetu juu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya kulipia dhambi Bwana alijua ya kwamba wakati mwingine tungejisikia woga. Nimelipitia hilo vivyo hivyo na wewe pia. … Katika Kanisa hili tunaweza tukawa wachache kwa idadi kulingana na jinsi dunia inavyohesabu ushawishi, lakini tunapofungua macho yetu ya kiroho, ‘walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao’ [2 Wafalme 6:16]” (“Usifadhaike,” Liahona, Nov. 2018, 18, 19). Ni kwa jinsi gani ungetumia maneno haya kumsaidia mtu anayehisi wasiwasi au hofu?

Ona pia “Dearest Children, God Is Near You,” Nyimbo za Dini, na. 96.

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

2 Wafalme 4

Mungu anaweza kufanya miujiza katika maisha yangu.

  • Baada ya kuwasaidia watoto wako waelewe muujiza ni nini, waalike waorodheshe mifano mingi ya miujiza kadiri wanavyoweza. Picha katika Kitabu cha Sanaa za Injili au Njoo, Unifuate zinaweza kusaidia. Kisha wangeweza kutafuta miujiza katika 2 Wafalme 4:1–7, 14–17, 32–35, 38–44. Je! Miujiza hii inafundisha nini kuhusu Baba wa Mbinguni?

  • Wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi Mungu ameonyesha upendo Wake kupitia miujiza. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kama vile “God’s Gracious Love” (Maktaba ya Injili).

Mtumishi kijana wa Kiisraeli anashuhudia kwa mke wa Naamani

Simama kama Shahidi, na Kwani Povi Winder

2 Wafalme 5:1–15

Ninaweza kuchagua kufanya kile Mungu anachoamuru kupitia nabii Wake.

  • Wasaidie watoto wako wajifunze hadithi katika 2 Wafalme 5:1–3, 9–14. Fikiria kutumia “Elisha Anamponya Naamani” (katika Hadithi za Agano la Kale, 134–37) au picha ya Naamani katika muhtasari wa wiki hii. Kwa nini Naamani hakutaka kuoga katika Mto Yordani, hata ingawa Elisha alimwambia kwamba hii ingemponya ugonjwa wake. Naamani alibarikiwa vipi alipofuata maelekezo ya Elisha? Ungeweza kushiriki na kila mmoja uzoefu wa wakati ulipomtii Bwana, hata wakati haukuwa na uhakika kwamba ulitaka kufanya hivyo.

    1:52

    Elisha Heals Naaman

  • Unaweza pia kusisitiza 2 Wafalme 5:13, ambapo watumishi wa Naamani walimsaidia kuamua kumtii nabii Elisha. Watoto wako kisha wangeweza kuzungumza kuhusu njia wanazoweza kuwasaidia marafiki zao au wanafamilia wao kumsikilza na kumtii nabii.

2 Wafalme 6:8–17

Mimi siko peke yangu.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kufikiria kwamba umezungukwa na jeshi lenye panga, farasi, na magari ya kukokotwa na farasi. Ungejhisi vipi? Ungefanya nini? Watoto wako kisha wangeweza kufumba macho yao wakati unawasomea 2 Wafalme 6:16–7 . (Ona pia “Elisha na Jeshi la Bwana,” katika Hadithi za Agano la Kale, 138–39, au picha mwishoni mwa muhtasari huu.) Wakati unapofika kwenye maneno “fumbua macho yake,” (mstari wa 17) waombe watoto wafumbue macho yao. Zungumza kuhusu kile mtumishi alichokiona. Shiriki na watoto wako njia ulizohisi kwamba Bwana alikuwa pamoja nawe wakati wa changamoto zako, hata wakati ilipoonekana kama uko peke yako.

    1:9

    Elisha and the Lord’s Army

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Elisha na mvulana wakitazama magari ya moto

“Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao,” na Stacy Minch

ukurasa wa shughuli za Msingi: Ninaweza kuchagua kufanya kile ambacho Mungu ameamuru kupitia nabii Wake.