2025
Kwa nini Bwana ana Kanisa?
Oktoba 2025 Liahona


Ujumbe wa kila mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana , Oktoba 2025

Kwa nini Bwana ana Kanisa?

wasichana

Lengo la Kanisa la Kristo ni "kuwawezesha watu binafsi na familia kumsaidia Mungu katika kutimiza kazi Yake ya wokovu na kuinuliwa." Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho husaidia "kuwastahilisha watoto wa [Mungu] kwa ajili ya daraja la juu zaidi la utukufu, ambayo ni kuinuliwa au uzima wa milele."

"Mwokozi … alilipatia mamlaka [Kanisa] ili kutimiza makusudi Yake—kuhubiri injili Yake, kutoa ibada na maagano Yake, na kufanya iwezekane kwa nguvu Zake kutuhalalisha na kututakasa."

Waumini wa Kanisa wanaweza kupata nguvu na baraka za Yesu Kristo kupitia mamlaka na funguo za ukuhani, maagano na ibada, mwongozo wa kinabii, maandiko, na jumuiya ya Watakatifu.

Kanisa pia limeamriwa: "Inukeni na mng’ae, ili nuru yako ipate kuwa bendera kwa ajili ya mataifa" (Mafundisho na Maagano 115:5).

Waumini wa Kanisa wanajitahidi "kung’ara" kwa kuishi injili, kuwaalika wote kupokea injili, kuunganisha familia milele, na kuwatunza masikini na wenye uhitaji. Hii ni kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa.