“Mnara wa Babeli,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Mnara wa Babeli,” Hadithi za Agano la Kale
Mwanzo 11
Mnara wa Babeli
Watu wakijaribu kujenga njia ya kufika mbinguni
Baada ya gharika, watu wakaanza kutokumtii Mungu. Baadhi yao hawakuamini mpango wa Mungu. Bila kumwuliza Mungu, wao walianza kujenga mnara ili kujaribu kufika mbinguni. Lilikuwa hekalu la uongo lililoitwa Mnara wa Babeli.
Mwanzo 11:4, 9
Mungu hakufurahi kuona watu wakijenga mnara. Akabadilisha lugha yao ili wasiweze kuelewana. Kwa sababu hawakuweza kuelewana, ilibidi waache kujenga mnara huo.
Mwanzo 11:6–8; Etheri 1:33
Mungu akawatawanya watu wale na kuwapeleka kote duniani kuishi.
Mwanzo 11:9