Wasichana
Majukumu


wasichana wakitabasamu

Wito Wangu Kama Katibu wa Darasa la Wasichana

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la wasichana

Kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Kinawasaidia wasichana kuwa wafuasi wa maisha yote wa Yesu Kristo kadiri wanavyofanya na kushika maagano matakatifu na kuongeza uongofu wao. Katika madarasa na mikusanyiko yao, wasichana wanawatumikia wengine, wanatimiza majukumu ya kimaagano, wanajenga umoja na wanajifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 11.1.1.)

Katibu wa Darasa la Wasichana

Katibu wa darasa la Wasichana anausaidia urais wa darasa na viongozi wa Wasichana kuwatumikia au kuwahudumia washiriki wa darasa. Anatayarisha ajenda kwa ajili ya mikutano ya urais, anaandika mihutasari, na kutunza kumbukumbu na mahudhurio katika mikutano ya Jumapili (11.3.4.2).

Mikutano ya Urais

Urais wa darasa la Wasichana hukutana mara kwa mara na wanaungana na katibu wa darasa na viongozi watu wazima wa Wasichana waliopangiwa kuwasaidia. Wanashauriana pamoja na kutafuta ufunuo kuhusu mapenzi ya Bwana kwa ajili ya darasa lao. Mikutano hii inaweza kujumuisha majadiliano juu ya kuwahudumia washiriki wa darasa, ikiwa na umakini maalumu katika kuwasaidia waumini wapya na kuwafikia waumini wasioshiriki kikamilifu, na kupanga mikutano ya darasa, huduma na shughuli. (Ona 11.3.4.3.)

Miongozo na Sera

Kwa miongozo na sera za ziada, ona sehemu ya 11.6 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla.