2025
Tunamfuata Yesu Kristo kwa Kuungana Naye katika Kazi Yake.
Juni 2025


“Tunamfuata Yesu Kristo kwa Kuungana Naye katika Kazi Yake,” Liahona, Juni 2025.

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Liahona, Juni 2025

Tunamfuata Yesu Kristo kwa Kuungana Naye katika Kazi Yake.

Tunashiriki katika kazi ya Mwokozi tunapofokasi kwenye madhumuni Yake, kutii amri Zake, na kupendana.

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala

Maelezo kutoka Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofman

Tunapobatizwa, tunaanza mchakato wa kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo. Sehemu ya mchakato huu inaashiria kwamba tunajiunga na Mwokozi katika kazi Yake. Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, aliandika, “Mojawapo ya maana muhimu ya kujichukulia juu yetu jina la Kristo [ni] utayari na sharti la kujichukulia juu yetu kazi ya Mwokozi na ufalme Wake.”

Kazi ya Mwokozi ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39). Kutokufa ni zawadi ya Yesu Kristo isiyo na masharti ambayo tayari imehakikishwa kupitia Ufufuko Wake. Uzima wa milele, hata hivyo, siyo sawa sawa na kutokufa. Uzima wa milele ni zawadi kuu ambayo Mungu anaweza kuwapa wanadamu (ona Mafundisho na Maagano 14:7). Ni kuishi milele kama familia katika uwepo Wake. Kwetu sisi kupokea uzima wa milele, lazima tuwe wanafunzi waaminifu wa Yesu Kristo. Hii inamaanisha tunapokea injili ya urejesho kwa kuwa na imani katika Mwokozi na Upatanisho Wake, kutubu, kubatizwa, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kufanya na kushika maagano ya hekaluni, na kuvumilia hadi mwisho. Kuvumilia hadi mwisho kunajumuisha kuungana na Mwokozi katika kazi Yake.

Kujishughulisha kwa Shauku

Tunashiriki katika kazi ya Mwokozi tunapowasaidia watoto wa Mungu pia kuwa wanafunzi waaminifu wa Yesu Kristo. Hii inajumuisha kushiriki injili Yake, kwa hivyo kukusanya Israeli waliotawanyika, kwa kutimiza majukumu katika Kanisa la Mwokozi na kwa kujitahidi kuwa kama Yeye. “Ufanisi wetu [katika kazi Yake] hautegemei jinsi wengine wanavyochagua kuitikia, mialiko yetu, au vitendo [vyetu] vya ukarimu wa dhati.” Rais Rais Russell M. Nelson alithibitisha: “Wakati wo wote unapofanya kitu cho chote ambacho kinachomsaidia mtu ye yote—upande wo wote wa pazia—kuchukua hatua kuelekea kufanya maagano na Mungu na kupokea ibada zao muhimu za ubatizo na za hekaluni, unasaidia katika kukusanya Israeli.”

Kuifanya kazi ya Mwokozi kuwa kazi yetu, tunafokasi kwenye madhumuni Yake, kutii amri Zake, na kupendana. Wakati tunapofanya kazi Yake kwa njia Yake (ona Mafundisho na Maagano 51:2), baadhi ya mambo yanaachwa kwa ajili yetu kufikiria sisi wenyewe. Mwokozi aliwaambia Watakatifu waliokusanyika katika Wilaya ya Jackson, Missouri:

“Kwani tazama, si vyema kwamba niamuru katika mambo yote; kwani yule alazimishwaye katika mambo yote, huyo ni mvivu na siyo mtumishi mwenye busara; kwa hiyo hapokei thawabu yoyote.

“Amini ninawaambia, wanadamu yawapasa kujishughulisha kwa shauku katika kazi njema, na kufanya mambo mengi kwa hiari yao wenyewe, na kutekeleza haki nyingi;

“Kwani uwezo upo ndani yao, ambamo wao ni mawakala juu yao wenyewe. Na kadiri wanadamu watakavyofanya mema hawatakosa thawabu zao” (Mafundisho na Maagano 58:26–28)

Tunapomfuata Mwokozi, tunapoungana Naye katika kazi Yake, na kuwasaidia wengine kuwa wanafunzi Wake waaminifu, tunafundisha kile ambacho Yeye angefundisha. Kwa sababu haturuhusiwi kufundisha kitu kingine cho chote (ona Mafundisho na Maagano 52:9, 36)), tunafokasi bila kuchepuka juu ya mafundisho Yake (ona Mafundisho na Maagano 68:25). Kwa nyongeza, tunawazingatia hasa wale ambao ni maskini, wenye uhitaji, na walio katika mazingira hatarishi (ona Mafundisho na Maagano 52:40). Msisitizo huu uliwekwa wazi wakati Mwokozi aliponukuu kutoka kwa Isaya katika sinagogi huko Nazareti:

“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa,

“Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:18–19; ona pia Isaya 61:1–2).

Mwaka unaokubaliwa wa Bwana unataja wakati ambapo baraka zote za agano la Mungu zitakapokuwa zimerundikwa juu ya watu Wake. Tunamfuata Yesu Kristo kwa kuwaalika wengine kupokea baraka za kufanya na kushika maagano na Mungu na kwa kuwajali wale walio maskini au vinginevyo walio na uhitaji.

Kuungana na Yesu Kristo katika kazi Yake ni ya kufurahisha kwa sababu kazi Zake, miundo, na madhumuni Yake “hayawezi kuvurugwa, wala hayawezi kuwa bure” (Mafundisho na Maagano 3:1). Kwa wale wanaohisi kuvunjika moyo, Bwana alishauri: “Kwa hiyo, msichoke katika kutenda mema, kwa maana mnaweka msingi wa kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu” (Mafundisho na Maagano 64:33). Tunamruhusu Bwana kushughulikia mavuno, na kwa urahisi tunafanya sehemu yetu.

Moyo na Akili Yenye Kukubali

Kufanya sehemu yetu ni rahisi kuliko tunavyoweza kufikiria kwa sababu hatuhitaji kuleta talanta za ajabu au uwezo kwenye kazi ya Bwana. Hitaji Lake ni rahisi tu kutia sharti na utayari. Bwana aliwaambia Watakatifu huko Kirtland, Ohio, “Tazama, Bwana anahitaji moyo na akili yenye kukubali” (Mafundisho na Maagano 64:34). Bwana anaweza kuwafanya wale walio tayari kuwa na uwezo, lakini hawezi au hatawafanya wale wanaoweza kuwa tayari. Kwa maneno mengine, kama tumeahidi na tuko radhi, Yeye anaweza kututumia. Lakini bila kujali tuna vipaji kiasi gani, Yeye hatatutumia sisi isipokuwa tumejikita kwenye kazi Yake na radhi kumsaidia Yeye.

Samuel na Anna-Maria Koivisto walionyesha vyote sharti na utayari. Mara baada ya ndoa yao, akina Koivisto walihama kutoka Jyväskylä, Finland, kwenda Göteborg, Uswidi, kutafuta fursa za kazi. Baada ya kuwasili, Kaka Koivisto alialikwa kuzungumza na Rais Leif G. Mattsson, mshauri katika urais wa Kigingi cha Göteborg Sweden. Kwa sababu Samuel hakuzungumza Kiswidi, usaili uliendeshwa kwa Kiingereza.

Kufuatia mazungumzo mafupi, Rais Mattsson alimwomba Samuel kuhudumu kama kiongozi wa kazi ya umisionari katika Kata ya Utby. Samuel alionyesha dhahiri: “Lakini mimi sizungumzi Kiswidi.”

Rais Mattsson aliegemea meza yake na kumuuliza kwa umakini, “Je, niliuliza kama ungeweza kuongea Kiswidi, au uko tayari kumtumikia Bwana?”

Samuel alijibu, “Uliuliza kama nilikuwa radhi kumtumikia Bwana. Nami niko tayari.”

Samuel alikubali wito huo. Anna-Maria pia alikubali miito. Wote walihudumu kwa uaminifu na kujifunza kuongea kiswidi kizuri katika mchakato huo.

Sharti na utayari wa kumtumikia Bwana unaelezea sifa za maisha ya Samuel na Anna-Maria. Wao ni mashujaa wa kawaida katika Kanisa. Wametumikia kwa uaminifu kila mara wanapoulizwa. Wamenifundisha kwamba tunapotumikia, tunatumia vipaji tulivyonavyo (ona Mafundisho na Maagano 60:13), na Bwana kisha anatusaidia kutimiza madhumuni Yake.

Tunapokuwa tayari kuhudumu, tunajitahidi kutolalamika au kunung’unika, kwa sababu hatutaki kufifisha huduma yetu kwa njia yo yote ile. Kulalamika kunaweza kuwa ishara ya msimamo wa kuyumbayumba, au kwamba upendo wetu kwa Mwokozi haufai kuwa hivyo. Kuachwa bila kukaguliwa, kunung’unika kunaweza kuendelea kwa uasi wa wazi dhidi ya Bwana. Maendeleo haya yanaonekana katika maisha ya Ezra Booth, mwongofu wa mwanzo wa Kanisa huko Ohio ambaye aliitwa kama mmisionari huko Missouri.

Alipokuwa akiondoka Ohio mnamo Juni 1831, Ezra alihudhika kwamba baadhi ya wamisionari waliweza kusafiri kwa gari la kukokotwa na maksai wakati yeye ilibidi atembee katika joto la majira ya joto, akihubiri njiani. Alinung’unika. Alipowasili Missouri, alihisi kushindwa. Missouri haikuwa kile alichotarajia. Badala yake, alitazama kote na kubainisha kwamba “matarajio yalionekana kuwa na huzuni kidogo.”

Ezra akawa anazidi kuwa mwenye kejeli, dhihaka na mkosoaji. Alipokuwa akiondoka Missouri, badala ya kuhubiri alipokuwa akienda, kama alivyoombwa kufanya, alirudi Ohio haraka kadiri alivyoweza. Manung’uniko yake ya awali yalibadilika na kuwa kuyumbayumba na hatimaye kupoteza kujiamini katika uzoefu wake wa kiroho wa mwanzo. Punde Ezra aliondoka Kanisani na “hatimaye ‘kuacha Ukristo na akawa mtu asiyeaminika.’”

Vivyo hivyo vinaweza kutokea kwetu kama hatuko makini. Kama hatuwezi kudumisha mtazamo wa milele, kujikumbusha wenyewe ni kazi gani hii hasa, tunaweza kulalamika, kuyumbayumba, na hatimaye kupoteza imani tuliyonayo.

Ninaomba kwamba tuweze kuchagua kumfuata Yesu Kristo kwa kuungana Naye katika kazi Yake. Tunapofanya hivyo, tunapewa “ahadi kubwa sana na za thamani” (2 Petro 1:4). Baraka hizi zinajumuisha msamaha wa dhambi (ona Mafundisho na Maagano 60:7; 61:2, 34; 62:3; 64:3), wokovu (ona Mafundisho na Maagano 6:13; 56:2), na kuinuliwa (ona Mafundisho na Maagano 58:3–11; 59:23). Ndiyo, tumeahidiwa zawadi kuu zaidi ambayo Mungu anaweza kuitoa—uzima wa milele.

Muhtasari

  1. Dallin H. Oaks, His Holy Name (1998), 37.

  2. Kukusanya Waisraeli kunaashiria kuwaalika wote kuwa waumini wa kweli katika Yesu Kristo.

  3. Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023), 13 Maktaba ya Injili.

  4. Russell M. Nelson, “Hope of Israel” (worldwide youth devotional, June 3, 2018), Maktaba ya Injili.

  5. Ona Matthew McBride, “Ezra Booth and Isaac Morley,” katika Revelations in Context: The Stories behind the Sections of the Doctrine and Covenants (2016), 130–36.