Ujumbe wa kila mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Februari 2025
Msaada kutoka Chanzo Kikamilifu
Bila kujali ni mapambano gani unayopingana nayo, Yesu Kristo atakusaidia unapomgeukia Yeye.
Mpangilio, na Jeanette Bourup
Wakati mmoja au mwingine sote tunahitaji msaada kidogo. Wakati mwingine msaada mwingi. Ukweli ni kwamba, maisha kwa kawaida huenda vizuri zaidi wakati unapokuwa haujaribu kuyaendea peke yako.
Yesu Kristo ndiye chanzo chako kikamilifu cha msaada, tumaini na nguvu. Anaweza pia kukubadilisha wewe kuwa bora—pengine hata katika njia ambazo hukufikiria inawezekana.
Badiliko la Moyo
Je, umewahi kuomba kwamba Mungu alainishe mioyo ya maadui zako? Kama ndivyo, uko katika kundi zuri (ona 3 Nefi 12:44; Moroni 7:48). Hata kama huna maadui kwa namna hiyo hiyo ya Kitabu cha Mormoni (unajua, maadui waliojihami kwa silaha na tayari kushambulia), pengine umeomba kwamba Mungu alainishe moyo wa mtu ambaye hakuwa anakutendea vizuri.
Lakini je, umewahi kufikiria kusali na kumwomba Mungu aulainishe moyo wako? Labda unakuwa na wakati mgumu kumsamehe mtu. Au unaendelea kuwa na hasira, hata kama hutaki kufanya hivyo. Au unataka kuhisi ukarimu zaidi kwa ndugu zako licha ya ukweli kwamba wanakukasirisha wakati mwingine.
“[Yesu Kristo] ataubadilisha moyo wako na maisha yako. Kidogo kidogo, utakua na kuwa zaidi kama Yeye. Muunganiko wako wa agano na Yeye utakuletea ufikiaji mkubwa kwenye nguvu Zake” (Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi [2022], 8, msisitizo umeongezwa).
Je, hiyo sio ahadi kubwa? Bila kujali unapambana na nini, hata moyo wako mwenyewe, Yesu Kristo anaweza kusaidia. Ni kwa jinsi gani unaweza kumgeukia Yeye leo?
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, February 2025. Swahili. 19621 743