2023
Yesu Ndiye Nuru Yangu ya Kweli
Januari 2023


Ninaweza Kupiga Wimbo Huo!

Kwani Yesu ni Nuru

Kwa uchangamfu [robo noti]=116–126

1. Usiku giza likijaza chumba changu,

Sihitaji kuwa na woga.

Ninafikiria upendo wa Kristo

Na najua kwamba Yeye yu karibu,

2. Ninapojaribiwa kufanya kosa,

Ninatafuta nuru ya Mwokozi.

Na ninapofikiria yote Yeye amefanya,

Ninataka kufanya kile kilicho sahihi,

Kibwagizo: Kwani Yesu ndiye nuru yangu ya kweli.

Yeye hunilinda mchana na usiku.

Yeye hunisaidia kuchagua kilicho sahihi.

Nitafuata nuru Yake.