Nini kiko Akilini Mwako?
Je, Mwokozi bado ananipenda kama nikifanya uchaguzi mbaya?
—Wasiwasi katika Wellington
Mpendwa mwenye wasiwasi,
Yesu Kristo anakupenda kikamilifu. Kama ukifanya uchaguzi mbaya, Yeye bado anakupenda. Na anaweza kukusaidia kutubu na kurekebisha mambo tena. Yeye daima anakusubiri wewe umfuate Yeye. Anakuamini wewe! Na sisi pia tunakuamini.
Kata kadi hii na uiweke pamoja na maandiko yako. Unaweza kusoma mistari hii unapohisi wasiwasi au kukata tamaa.
Gazeti la Rafiki
Yesu Kristo Ananipenda
-
Yohana 14:18
-
Isaya 41:10
-
Wafilipi 4:13
-
Warumi 8:38–39
-
Yohana 14:27
Kielelezo cha Kristo na Kristin Kwan