“Mikutano ya Baraza la Mwalimu—Kwa Ajili ya Wazazi na Walimu Walioitwa,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)
“Mikutano ya Baraza la Mwalimu,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi
Mikutano ya Baraza la Mwalimu—Kwa Ajili ya Wazazi na Walimu Walioitwa
Kila kata inapaswa kuwa na mikutano ya baraza la walimu kila robo mwaka, kwa wote wazazi na kwa walimu walioitwa katika kata. Katika mikutano hii, wazazi na walimu wengine wanaweza kushauriana pamoja kuhusu kanuni za kufundisha kama Kristo (ona Kitabu cha Maelekezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 13.4, 13.5, 17.4, 17.5, Gospel Library).
Aina zote mbili za mikutano ya baraza la mwalimu hufanyika mara moja katika robo mwaka wakati wa dakika 50 za darasa siku ya Jumapili.
Mikutano ya Baraza la Mwalimu Kwa Ajili ya Wazazi
Ni Nani Huongoza Mikutano Hii? Kwa kawaida, mshiriki wa urais wa Shule ya Jumapili, huongoza mikutano hii ya baraza la mwalimu. Hata hivyo, uaskofu unaweza kuwapangia waumini wengine wa kata kuongoza mikutano wakati mwingine.
Baraza la kata, likiwa na usaidizi kutoka kwa urais wa Shule ya Jumapili, husimamia mikutano ya baraza la mwalimu kwa ajili ya wazazi. Wanashauriana pamoja kuhusu mahitaji ya wazazi na familia, na wanafanya kazi pamoja kuamua kanuni zipi kutoka Kufundisha katika Njia ya Mwokozi zitakidhi vyema mahitaji hayo.
Ni Nani Anapaswa Kuhudhuria? Baraza la kata linaamua kama linawaalika wazazi mahususi au kuweka mahudhurio wazi kwa wote wanaotaka kushiriki.
Ni Wakati Gani Mikutano Hii Inapoaswa Kufanyika? Mikutano ya baraza la walimu kwa ajili ya wazazi inaweza kufanyika Jumapili yoyote, kama itakavyoamuliwa na baraza la kata.
Mikutano ya Baraza la Mwalimu kwa Ajili ya Walimu Walioitwa
Ni Nani Huongoza Mikutano Hii? Kwa kawaida, mshiriki wa urais wa Shule ya Jumapili, huongoza mikutano ya baraza la mwalimu kwa ajili ya walimu walioitwa. Hata hivyo, uaskofu unaweza kuwapangia waumini wengine wa kata kuongoza mikutano wakati mwingine.
Baraza la kata, likiwa na usaidizi kutoka kwa urais wa Shule ya Jumapili, husimamia mikutano ya baraza la mwalimu kwa ajili ya walimu walioitwa. Wanashauriana pamoja kuhusu mahitaji ya walimu na wanafunzi, na wanafanya kazi pamoja kuamua ni kanuni zipi kutoka Kufundisha katika Njia ya Mwokozi zitakidhi vyema mahitaji hayo.
Ni Nani Anapaswa Kuhudhuria? Kila mtu anayefundisha akidi au darasa katika kata anapaswa kuhudhuria mikutano ya baraza la mwalimu. Washiriki wa urais wa akidi na kikundi wanaalikwa pia.
Ni Wakati Gani Mikutano Hii Inapaswa Kufanyika? Walimu wanahudhuria mikutano ya baraza la walimu siku ya Jumapili wakati hawafundishi darasa lao la kawaida.
-
Walimu wa akidi ya ukuhani, Muungano wa Usaidizi, na Wasichana wanaweza kuhudhuria mojawapo ya Jumapili ya kwanza au ya tatu, kama itakavyoamuliwa na viongozi wenyeji.
-
Walimu wa Shule ya Jumapili wanaweza kuhudhuria mojawapo ya Jumapili ya pili au ya nne, kama itakavyoamuliwa na viongozi wenyeji.
-
Walimu wa Watoto wanaweza kuhudhuria Jumapili yo yote, kama itakavyoamuliwa na urais wa Watoto na wa Shule ya Jumapili katika kata. Ikiwa itapendekezwa, Walimu wa darasa la Watoto wanaweza kukutana tofauti na walimu wengine ili washauriane kuhusu mahitaji ya kipekee ya watoto wanao wafundisha. Hii inaweza kutokea wakati wa dakika 20 za muda wa kuimba, kabla au baada ya mikutano ya kila Jumapili, au katika siku nyingine ya wiki. Zaidi ya mkutano mmoja wa baraza la walimu inaweza kufanyika katika robo mwaka kwa ajili ya walimu wa Watoto, ili kwamba wote wasikose madarasa ya Watoto katika wiki hiyo. (Kumbuka: Kama itakavyohitajika, urais wa Darasa la Watoto huwateua walimu mbadala, huunganisha madarasa, au kufanya mipango mingine ili kuwaruhusu walimu wa Watoto kuhudhuria mikutano ya baraza la mwalimu.)
Umbizo la Mikutano
Mikutano ya baraza la mwalimu—kwa ajili ya wazazi na kwa walimu walioitwa—hufuata mfumo huu:
-
Shiriki na mshauriane pamoja (takribani dakika 20). Waalike wazazi au walimu kushiriki kile kinachofanya kazi vyema wanapofundisha injili nyumbani au katika madarasa yao. Wangeweza pia kushiriki changamoto wanazokabiliana nazo au vitu ambavyo wangependa kuboresha.
-
Jifunzeni pamoja (takribani dakika 15). Jadili na wazazi au walimu mojawapo ya kanuni katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi. Njoo, Unifuate inaweza pia kutumika kama nyenzo kwa ajili ya majadiliano haya.
-
Panga na kualika (takribani dakika 10). Waalike wazazi au walimu kushiriki kile walichojifunza wakati wa mkutano na jinsi wanavyopanga kukitumia.