Kuwaimarisha Waumini Wapya
Itakase Siku ya Sabato


“Itakase Siku ya Sabato,” Njia Yangu ya Agano (2020)

“Itakase Siku ya Sabato,” Njia Yangu ya Agano

darasa la Kanisa

Itakase Siku ya Sabato

Kila Jumapili una nafasi ya kuonyesha upendo wako kwa Mungu kwa kile unachofanya siku hiyo. Unaonyesha upendo huu kwa kuhudhuria kanisani, kupokea sakramenti na kuwahudumia wengine. Unapopokea sakramenti, unakumbuka dhabihu ya Yesu Kristo na kufanya upya maagano matakatifu uliyoyafanya wakati wa ubatizo.

  • Jifunze juu ya umuhimu wa kupokea sakramenti kila wiki, kutoa ushuhuda wako, na kuitakasa siku ya Sabato. Fikiria kutumia:

    • 3 Nefi 18:1–12 (pia ona Mathayo 26:26–28; Marko 14:22–25; Luka 22:19–20; Mafundisho na Maagano 20:77, 79).

    • Mada na Maswali, “Ushuhuda,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

    • Kuabudu Siku ya Sabato” katika Kujifunza na Kuhudumu ndani ya Kanisa (kijitabu, 2016), 5–9.

  • Kutoa ushuhuda wako hukusaidia kuufanya uwe imara! Fikiria kutoa ushuhuda wako katika mkutano ujao wa ushuhuda.