Wito wangu kama Rais wa Darasa la Wasichana
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Wasichana
Kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Kinawasaidia wasichana wawe wafuasi wa maisha yote wa Yesu Kristo kadiri wanavyofanya na kushika maagano matakatifu na kuongeza uongofu wao. Katika madarasa na mikusanyiko yao, wasichana wanawatumikia wengine, wanatimiza majukumu ya kimaagano, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 11.1.1.)
Rais wa darasa la Wasichana
Marais wa darasa huongoza juhudi za darasa kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa, kupata kumjua na kumtumikia kila msichana, kupanga na kuendesha mikutano ya darasa ya Jumapili na shughuli zinginezo, kushiriki katika juhudi za kata za kushiriki injili, na kushiriki katika juhudi za hekaluni na historia ya familia (ona 11.3.4.2). Washauri wake wanamsaidia.
Mikutano ya Urais
Urais wa darasa la Wasichana hukutana mara kwa mara na wanaungana na viongozi watu wazima wa Wasichana waliopangiwa kuwasaidia. Wanashauriana pamoja na kutafuta ufunuo kuhusu mapenzi ya Bwana kwa ajili ya darasa lao. Mikutano hii inaweza kujumuisha majadiliano juu ya kuwahudumia washiriki wa darasa, ikiwa na umakini maalumu katika kuwasaidia waumini wapya na kuwafikia waumini wasioshiriki kikamilifu, na kupanga mikutano ya darasa, huduma, na shughuli. (Ona 11.3.4.3.)
Baraza la Vijana la Kata
Baraza la vijana la kata linajadili njia za kuwasaidia wengine wajenge shuhuda, wapokee ibada okozi, washike maagano, na wawe wafuasi waliowekwa wakfu wa Yesu Kristo. Wanashauriana pamoja kuhusu mahitaji ya wasichana na wavulana katika kata. Wanaweza kujadili shughuli ili kukidhi mahitaji haya. (Ona 11.3.4.4.)
Miongozo na Sera
Kwa miongozo na sera za ziada, ona sehemu ya 11.6 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla.