Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Darasa la Wasichana
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Wasichana
Kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu kujiandaa kurudi katika uwepo Wake. Inawasaidia wasichana kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kwa maisha yote wanapofanya na kushika maagano matakatifu na kuzidisha kina cha uongofu wao. Katika madarasa yao, na mikusanyiko, wasichana wanawatumikia wengine, wanatimiza majukumu ya kimaagano, kujenga umoja, na kujifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 11.1.1.)
Mshauri katika Darasa la Wasichana
Rais wa darasa na washauri wake wanaongoza juhudi za darasa za kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa, kupata kujuana na kutumikiana wao kwa wao, kupanga na kuendesha mikutano ya darasa la Jumapili na shughuli zingine, kushiriki katika juhudi za kata za kuhubiri injili, na kushiriki katika juhudi za kazi ya hekalu na historia ya familia (ona 11.3.4.2).
Mikutano ya Urais
Urais wa darasa la Wasichana hukutana mara kwa mara na wanaungana na viongozi watu wazima wa Wasichana waliopangiwa kuwasaidia. Wanashauriana pamoja na kutafuta ufunuo kuhusu mapenzi ya Bwana kwa darasa lao. Mikutano hii inaweza kujumuisha majadiliano juu ya kuwatumikia washiriki wa darasa, na umakini maalum katika kuwasaidia waumini wapya na kuwafikia waumini wasio shiriki kikamilifu, na kupanga mikutano ya darasa, huduma, na shughuli. (Ona 11.3.4.3.)
Miongozo na Sera
Kwa ziada kuhusu miongozo na sera, ona sehemu ya 11.6 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla.