Wito wangu kama Mwalimu wa Shule ya Jumapili
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Kusudi la Shule ya Jumapili
Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Inafanya hivi kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 13.1).
Walimu wa Shule ya Jumapili
Walimu wa Shule ya Jumapili hupaswa kuwajua washiriki wa darasa, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawahudhurii madarasa. Walimu wanawasaidia waumini katika juhudi zao za kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona 13.2.3). Walimu wanaongozwa na urais wa Shule ya Jumapili wa kata na kuhudhuria mikutano ya baraza la walimu kila robo mwaka (ona 17.4).
Madarasa ya Shule ya Jumapili
Madarasa ya Shule ya Jumapili yanafanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi. Yanadumu kwa muda wa dakika 50. Ukubwa wa darasa hutofautiana kulingana na mahitaji ya kila kata. Ili kujiandaa kufundisha, walimu wa Shule ya Jumapili hutumia maandiko na masomo yaliyopangwa katika Njoo, Unifuate (ona 13.3).
Kanuni za Ufundishaji Kama wa Kristo
Kufundisha katika njia ya Mwokozi ni jukumu aminifu na takatifu. Unapofundisha injili, fuata mfano wa Mwokozi, ambaye ni Mwalimu Mkuu. Walimu wa Shule ya Jumapili hufuata kanuni katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi na sura ya 17 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla (ona 17.1).
Kujifunza Injili ambako kiini chake ni Nyumbani
Ili kuwa mwongofu kwa Bwana Yesu Kristo, kila muumini wa Kanisa anawajibika kujifunza injili wao wenyewe. Viongozi na walimu wanawajibika kuwahimiza waumini kutafuta mwongozo wao wenyewe wa kiungu kuhusu jinsi gani ya kujifunza na kufundisha injili (ona 17.2).