Wasichana
Majukumu


wasichana wakitabasamu

Wito wangu kama Rais wa Wasichana katika kigingi

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la kikundi cha Wasichana

Kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Kinawasaidia wasichana kuwa wafuasi wa Yesu Kristo wa maisha yote kadiri wanavyofanya na kushika maagano matakatifu na kuongeza kina cha uongofu wao. Katika madarasa na mikusanyiko yao, wasichana wanawahudumia wengine, wanatimiza majukumu ya kimaagano, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelekezo ya Jumla, 11.1.1.)

Rais wa Wasichana katika Kigingi

Rais wa Wasichana katika Kigingi huandaa “jeshi la vijana” wa Bwana ili kuikusanya Israeli kupitia kushiriki katika juhudi za kujenga imani na kuwaimarisha watu binafsi (ona Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Hope of Israel” [worldwide youth devotional, June 3, 2018], Gospel Library). Anahudumu katika baraza la kigingi na kamati ya uongozi ya vijana katika kigingi (ona 6.7.1.2).

Mikutano

Rais wa Wasichana katika Kigingi hutoa mafunzo kwa urais wa vikundi katika kata wakati wa mikutano ya mwaka ya uongozi katika kigingi (ona 29.3.4), anahudhuria mikutano ya urais na mikutano ya baraza la uratibu pale anapoalikwa na Sabini wa Eneo (ona 29.4), na huzungumza katika mikutano ya sakramenti na mahali pengine wakati anapoalikwa na urais wa kigingi.

Shughuli

Chini ya maelekezo ya urais wa kigingi, urais wa Wasichana katika kigingi pia utapanga na kuratibu shughuli na kambi za Wasichana katika kigingi (ona 6.7.1.2). Kwa vigingi vingi, urais hushauriana kwa pamoja ili kupendekeza shughuli za pamoja kwa urais wa kigingi (ona 20.3.1).

Miongozo na Sera

Miongozo na sera za ziada vinapatikana katika sehemu ya  11.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.