Wito wangu kama Katibu wa Shule ya Jumapili katika Kigingi
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Kusudi la Shule ya Jumapili
Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 13.1).
Katibu wa Shule ya Jumapili katika Kigingi
Chini ya maelekezo ya rais wa Shule ya Jumapili katika kigingi, majukumu ya katibu yanajumuisha kuandaa ajenda za mikutano, kuandika na kufuatilia majukumu katika mikutano ya urais, kuweka kumbukumbu zingine, kuandaa ripoti kama maombi ya urais, na kusaidia kuandaa bajeti ya mwaka (ona 6.7.3).
Mikutano na Mabaraza
Urais wa Shule ya Jumapili wa kigingi na katibu shauriana kwa pamoja mara kwa mara (ona 29.3.4).
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera inapatikana katika sehemu ya 13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.