Shule ya Jumapili
Majukumu


mtu anafundisha darasa

Wito wangu kama Rais wa Shule ya Jumapili wa Kigingi

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Kusudi la Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 13.1).

Rais wa Shule ya Jumapili wa Kigingi

Majukumu ya urais wa Shule ya Jumapili wa kigingi yanajumuisha kufanya kazi ya kujenga imani na kuimarisha watu binafsi na familia katika kigingi, kuelekeza majukumu ya urais mpya wa Shule ya Jumapili katika kata, na kutoa usaidizi na maelekezo endelevu (ona 6.7.1). Washauri pia wanamsaidia rais wa Shule ya Jumapili wa kigingi katika kazi za ziada.

Mikutano na Mabaraza

Urais wa Shule ya Jumapili wa kigingi hushauriana pamoja mara kwa mara. Wanapanga na kuendesha mikutano ya uongozi katika kigingi ili kuwafundisha viongozi wa Shule ya Jumapili katika kata majukumu yao, kuwasaidia kujiboresha kama viongozi na walimu, na kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo (ona 29.3.4).

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera vinapatikana katika sehemu ya 13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.