Shule ya Jumapili
Majukumu


mtu akifundisha darasa

Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Shule ya Jumapili ya Kigingi

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kutumikia katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Kusudi la Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 13.1).

Mshauri katika Shule ya Jumapili ya Kigingi

Majukumu ya urais wa Shule ya Jumapili ya kigingi yanajumuisha kufanya kazi ya kujenga imani na kuimarisha watu binafsi na familia katika kigingi, kuelekeza urais mpya wa Shule ya Jumapili ya kata, na kutoa msaada na maelekezo endelevu (ona 6.7.1). Washauri pia wanatoa msaada kwa rais wa Shule ya Jumapili ya kigingi katika majukumu ya ziada.

Mikutano na Mabaraza

Urais wa Shule ya Jumapili ya Kigingi hushauriana pamoja mara kwa mara. Wanapanga na kuendesha mikutano ya uongozi ya kigingi ili kuwafundisha viongozi wa Shule ya Jumapili ya kata majukumu yao, kuwasaidia kujiboresha kama viongozi na walimu, na kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo (ona 29.3.4).

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera inapatikana katika sehemu ya  13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.