Wito Wangu kama Mwalimu wa Muungano wa Usaidizi
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Muungano wa Usaidizi
Muungano wa Usaidizi ni kikundi kitakatifu kilichoanzishwa kwa ajili ya wanawake wote watu wazima katika Kanisa. Muungano wa Usaidizi huwasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kuondoa mateso”—kwa kutoa faraja ya Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 9.1).
Walimu wa Muungano wa Usaidizi
Walimu huitwa ili kuwasaidia watu waimarishe imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Walimu wa Muungano wa Usaidizi huwaunga mkono urais. Urais wa Muungano wa Usaidizi kwa sala huchagua jumbe za kufundisha kulingana na mahitaji ya akina dada (ona 9.2.1.2).
Mikutano ya Jumapili
Muungano wa Usaidizi hukutana kila Jumapili ya pili na ya nne kwa lengo la kuongeza imani katika Yesu Kristo, kujenga umoja na kuimarisha familia na nyumba. Mikutano huanza kwa sala na hujumuisha muda wa kushauriana pamoja na maelekezo na mjadala wa kiinjili uliojikita kwenye mahubiri ya mkutano mkuu wa hivi karibuni (ona 9.2.1.2).
Kanuni za Ufundishaji Kama wa Kristo
Kufundisha katika njia ya Mwokozi ni uaminifu na jukumu takatifu. Unapofundisha injili, fuata mfano wa Mwokozi, ambaye ni Mwalimu Mkuu. Walimu wa Muungano wa Usaidizi hufuata kanuni katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi na sura ya 17 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla (ona 17.1).
Kujifunza Injili ambako kiini chake ni Nyumbani
Wakati waumini wanapojifunza na kuishi injili nyumbani, uongofu wao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo huwa wa kina. Viongozi wa Muungano wa Usaidizi huwahimiza akina dada kujifunza maandiko na maneno ya manabii walio hai, binafsi na pamoja na familia zao (ona 17.2).