“35. Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“35. Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
35.
Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano
35.1
Dhumuni
Kanisa hutoa nyumba za mikutano ili kwamba wote wanaoingia waweze:
-
Kufanya na kufanya upya maagano kupitia ibada takatifu (ona Mafundisho na Maagano 20:75; 59:9–12).
-
Kukutana pamoja (ona 3 Nefi 18:22–23).
-
Kuabudu na kusali pamoja (ona Mosia 18:25; Moroni 6:9).
-
Kufundishana na kuhudumiana sisi kwa sisi (ona Moroni 6:4–5).
-
Kushiriki katika matumizi mengine yaliyoidhinishwa kama ilivyoelezwa katika sura hii.
35.2
Wajibu na Majukumu
35.2.2
Meneja wa Vifaa vya Kanisa
Meneja wa vifaa aliyeajiriwa na Kanisa anasaidia kila kigingi kuendesha nyumba za mikutano. Yeye anapanga ukarabati mkubwa, usafi wa kina, na matengenezo ya kawaida ya jengo.
Kadiri inavyohitajika, meneja wa vifaa anasaidia kuwaelekeza wawakilishi wa majengo ya kigingi na kata juu ya jinsi ya kusafisha jengo na kufanya kazi zingine za eneo husika. Yeye anatoa maelekezo, nyenzo na vifaa.
Yeye anaweza pia kurejea upya gharama za jengo akiwa pamoja na uaskofu.
35.2.7
Uaskofu
Uaskofu (au mwakilishi wa jengo katika kata) anawafundisha waumini jinsi ya kutumia, kutunza, na kulilinda jengo. Uaskofu pia unagawa funguo za jengo kwa viongozi wa kata.
Wanahakikisha kwamba shughuli katika jengo na kwenye viwanja zinaendeshwa kwa usalama (ona 20.7).
Wanawasiliana na meneja wa vifaa wa Kanisa kuhusu matengenezo na mahitaji ya kiuendeshaji. Wanaweza pia kurejelea upya matumizi yanayohusika wakiwa na meneja wa vifaa.
35.2.9
Mwakilishi wa Jengo wa Kata
Uaskofu ndiyo unaamua ikiwa wanahitaji kumwita mwakilishi wa jengo wa kata. Kama wanaamua kutoa wito huu, uaskofu unaweza kumwita mtu mzima nwanamume au mwanamke ambaye ni muumini. Kama mwakilishi wa jengo wa kata hakuitwa, askofu anaweza kutoa wajibu huu kwa mmoja wa washauri wake, karani wa kata au karani msaidizi wa kata, au katibu mtendaji.
Mwakilishi wa jengo wa Kata anawasimamia waumini na watu wanaojitolea kulisafisha na kulitunza jengo.
35.3
Kutoa Nyumba za Mikutano
Nyumba za mikutano zinatofautiana kwa ukubwa na aina kulingana na mahitaji na hali ya mahali husika. Nyumba ya mikutano inaweza kuwa imejengwa na Kanisa au nafasi iliyonunuliwa, nyumba ya muumini, shule ya eneo husika au kituo cha kijamii, nafasi iliyokodiwa, au uchaguzi mwingine ulioidhinishwa.
Viongozi wa eneo na viongozi wenyeji wanajitahidi kutumia kikamilifu nyumba za mikutano zilizopo na kuwa wenye hekima katika kupendekeza eneo la ziada.
35.4
Matunzo ya Nyumba za Mikutano
35.4.1
Kuzisafisha na Kuzitunza Nyumba za Mikutano
Viongozi wenyeji na waumini, ikijumuisha vijana, wanao wajibu wa kusaidia kuweka kila jengo liwe safi na katika hali nzuri.
Ratiba ya kusafisha haipaswi kuwa mzigo kwa waumini. Kwa mfano, kama kusafiri kwenda kwenye jengo ni changamoto, waumini wanaweza kulisafisha kama sehemu ya matukio ya wiki wakati wawapo tayari kwenye jengo.
35.4.2
Kuomba Ukarabati
Waumini wa baraza la kata na kigingi wanaweza kutoa taarifa ya mahitaji kwa ajili ya ukarabati wa jengo. Hii inaweza kufanywa kwa kutumia nyenzo ya Utoaji Taarifa juu ya Suala la Kifaa (FIR).
35.4.5
Usalama na ulinzi
Viongozi na waumini wanapaswa:
-
Kuacha wazi njia za kumbi, ngazi, milango ya kutokea, na vyumba vyenye vifaa vinavyotumika kwa ajili ya usalama wa kuingia na kutoka.
-
Kutotumia au kutunza vifaa hatarishi au vinavyoweza kuwaka moto katika majengo.
-
Kuanzisha na kufuata utaratibu wa kufunga na kufungua jengo.
-
Kuweka salama vifaa vinavyomilikiwa na Kanisa ili visiibiwe.
-
Kujua jinsi gani ya kufunga vitu kama vile bomba la maji, kuzima taa za umeme, gesi au mafuta.
Kadiri inavyohitajika, meneja wa vifaa anaweza kutoa ramani inayoonesha vifaa vya kuzima moto, visanduku vya huduma ya kwanza, na sehemu za kuzima vifaa. Taarifa za ziada kuhusu usalama zinapatikana katika “Taratibu za Usalama na za Ufungaji wa Milango” katika “Kutunza Nyumba za Mikutano” (Mwongozo wa Vifaa vya Nyumba ya Mikutano). Ona pia 20.7.
35.5
Sera juu ya Kutumia Nyumba za Mikutano za Kanisa
35.5.1
Kanuni na Mahitaji ya Msingi ya Kutumia Nyumba za Mikutano za Kanisa
Matumizi yote ya nyumba za mikutano za Kanisa lazima yatimize mahitaji ya msingi yafuatayo:
-
Yawe sawa na mafundisho, sera, na mazoea ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na asili takatifu na madhumuni matakatifu ya nyumba za mikutano za Kanisa.
-
Yawe ndani ya mipaka ya sheria.
-
Yawe sawa na hali ya msamaha wa kodi ya Kanisa pale inapohitajika.
-
Yachukue hatua zinazofaa kuepuka, kupunguza, na kudhibiti hatari za usalama, ikiwa ni pamoja na miongozo na sera za Kanisa zinazowalinda watoto na vijana (ona 12.5.1 na 20.7.1)
-
Yafuate masharti mengine na ukomo uliotolewa na rais wa kigingi au askofu.
35.5.2
Matumizi ya Kanisa ya Nyumba za Mikutano
Mikutano ya kanisa, programu, na shughuli zina kipaumbele juu ya matumizi mengine ya nyumba ya mikutano ikiwa kuna mgogoro.
Kata na vigingi vinaweza pia kutoa programu zingine za Kanisa ambazo zinawanufaisha waumini na jamii. Hizi zinajumuisha:
35.5.3
Matumizi ya Waumini ya Nyumba za Mikutano—Binafsi na Familia
Waumini wanaweza kuomba kutumia nyumba ya mkutano ndani ya kigingi chao kwa shughuli binafsi au za familia. Ili kupata idhini, wanawasiliana na mshiriki wa uaskofu wa kata inayokutana katika nyumba hiyo ya mikutano (au mtu anayemteua). Masharti yafuatayo yatumike:
-
Matumizi lazima yasimamiwe binafsi na mtu mzima anayewajibika wa kata inayokutana katika nyumba ya mikutano.
-
Watumiaji wana jukumu kamili kwa uharibifu wowote wa vifaa au jeraha lolote au uwajibikaji wowote unaohusiana na matumizi hayo.
-
Watumiaji lazima wasafishe na kurejesha vifaa kikamilifu kama vilivyokuwa kabla ya matumizi.
-
Watumiaji lazima wazingatie maelekezo na maombi kutoka kwa viongozi wa mahala husika, ikiwa ni pamoja na maombi ya viongozi kufuatilia matumizi.
-
Viongozi wa kanisa wanaweza kumwomba mtu yeyote au kikundi kuacha kutumia mali hiyo ikiwa hawafuati miongozo.
-
Kwa shughuli zilizoidhinishwa, viongozi wa kata na kigingi wanapaswa kufanya mipango ya upatikanaji wa nyumba ya mikutano. Funguo za jengo zinapaswa kutolewa tu kwa waumini wa kata au kigingi walioteuliwa.
Ona 38.3.4 kwa ajili ya matumizi ya nyumba za mikutano kwa ajili ya harusi na sherehe baada ya ndoa.
Ona 29.5 kwa ajili ya matumizi ya nyumba za mikutano kwa ajili ya mazishi na huduma zingine kwa marehemu.
35.5.4
Matumizi ya Nyumba za Mikutano za Kanisa kwa Mashirika Yasiyo ya Faida au kwa Vikundi Vingine au Watu Binafsi
Uongozi wa eneo unaweza kuruhusu mashirika yasiyo ya faida, jamii na vikundi vingine (kama vile timu za michezo), au watu binafsi ambao hawajaelezewa katika 35.5.3 kutumia nyumba za mikutano za Kanisa kwa shughuli au huduma nzuri. Masharti yaliyoorodheshwa katika 35.5.3 yanatumika.
Ili kupata idhini ya uongozi wa eneo kwa matumizi hayo, rais wa kigingi anawasiliana na meneja wa vifaa.
35.5.5
Dharura
Nyumba za mikutano za kanisa zinaweza kutumika kwa huduma muhimu ya jamii wakati wa dharura. Kwa mfano, rais wa kigingi anaweza kuruhusu nyumba za mikutano katika kigingi chake kutumiwa na mashirika ya maafa na wengine katika juhudi zinazohusiana (ona 35.5.4).
35.5.6
Matumizi ya Jengo Ambayo Hayaruhusiwi
35.5.6.1
Matumizi ya Kibiashara
Mali ya Kanisa haiwezi kutumika kwa madhumuni ya kibiashara. Matumizi kama hayo hayaendani na madhumuni ya mali za Kanisa. Yanaweza pia kuleta mgongano na sheria za mahali husika au za taifa ambazo zinaruhusu msamaha wa kodi kwa mali za Kanisa.
35.5.6.3
Madhumuni ya Kisiasa
Kanisa halifungamani na yeyote kisiasa. Mali ya Kanisa haiwezi kutumika kwa ajili ya madhumuni ya kisiasa au utetezi. Shughuli zilizopigwa marufuku ni pamoja na mikutano ya kisiasa na matumizi ya kampeni za kisiasa na vikundi vya utetezi.
Hata hivyo, kutumia mali kwa ajili ya usajili wa wapiga kura au kupiga kura kunaweza kuruhusiwa kama jambo la kipekee (ona 38.8.30). Rais wa kigingi anaweza kuomba ruhusa hii ya kipekee kutoka kwa meneja wa vifaa (ona 35.5.4).