“12. “Watoto,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“12. Watoto,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
12.
Watoto
12.1
Dhumuni na Muundo
Muundo wa kundi la Msingi unawasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake.
12.1.1
Dhumuni
Darasa la Watoto huwasaidia watoto:
-
Wahisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha.
-
Wajifunze kuhusu Yesu Kristo na wajibu wake katika mpango wa Baba wa Mbinguni.
-
Wajifunze na waishi injili ya Yesu Kristo.
-
Wahisi, watambue, na wafanyie kazi ushawishi wa Roho Mtakatifu.
-
Wajiandae kwa ajili ya, kufanya, na kuyashika maagano matakatifu.
-
Kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa.
12.1.3
Darasa la Watoto Wadogo
Darasa la watoto wadogo linawasaidia watoto wenye umri wa miezi 18 hadi miaka 3 wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha.
12.1.4
Madarasa
Wakati kuna watoto wa kutosha, wanagawanywa kwenye madarasa kutegemea umri wao.
Watoto kwa kawaida wanasonga mbele kutoka darasa la Watoto kwenda wasichana au akidi ya mashemasi katika Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12.
12.1.5
Muda wa Kuimba
Muda wa kuimba unawasaidia watoto wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha. Wakati watoto wanapoimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo.
Urais wa Watoto na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa na nyumbani.
12.1.6
Mawasilisho ya Watoto kwenye Mkutano wa Sakramenti
Mawasilisho ya mwaka ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti yanafanyika kipindi cha miezi michache ya mwisho ya mwaka.
Urais wa Watoto na kiongozi wa muziki kwa sala hupanga mawasilisho hayo. Uaskofu unatoa maelekezo. Watoto wanaweza kuimba, kuzungumza, na kushiriki hadithi, maandiko, au shuhuda.
12.1.7
Mkutano na Matayarisho ya Hekaluni na Ukuhani.
Urais wa Watoto unapanga mkutano wa Maandalizi ya Hekaluni na Ukuhani kila mwaka. Uaskofu unatoa maelekezo. Mkutano ni kwa ajili ya watoto wa umri wa miaka 10. Wazazi wanaalikwa.
12.2
Kushiriki katika Kazi ya Mungu ya Wokovu na Kuinuliwa
12.2.1
Kuishi Injili ya Yesu Kristo
12.2.1.2
Kujifunza Injili
Mikutano ya Watoto ya Jumapili. Mshiriki wa urais wa Watoto anaendesha ufunguzi.
Ratiba ni kama ifuatavyo:
|
Sehemu ya Mkutano |
Urefu |
|---|---|
Sehemu ya Mkutano Ufunguzi (sala, maandiko au Makala ya Imani, na mazungumzo—vyote vikitolewa na watoto) | Urefu Dakika 5 |
Sehemu ya Mkutano Muda wa kuimba | Urefu Dakika 20 |
Sehemu ya Mkutano Mabadiliko kwenda Madarasani | Urefu Dakika 5 |
Sehemu ya Mkutano Madarasa na sala ya kufunga | Urefu Dakika 20 |
Darasa la watoto wadogo kwa ajili ya watoto wa umri wa miezi 18 hadi miaka 3.linadumu kwa dakika 50. Tazama Watoto Wenu inatoa ratiba iliyopendekezwa.
12.2.1.3
Huduma na Shughuli
Kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 8, watoto wanaweza kuanza kuhudhuria shughuli za Watoto.
Shughuli za Watoto zinafanyika wakati wowote isipokuwa jioni za Jumapili au Jumatatu.
-
Shughuli za Watoto zinafanyika mara mbili kwa mwezi pale inapowezekana.
-
Wavulana na wasichana kwa kawaida hukutana mahali tofauti. Hata hivyo, wanaweza kuungana kwa shughuli fulani au katika sehemu zenye watoto wachache.
Uaskofu unahakikisha kwamba bajeti na shughuli kwa ajili ya wavulana na Wasichana katika darasa la Watoto zinatosha na zina usawa.
12.2.1.4
Maendeleo Binafsi
Katika juhudi zao za kuwa zaidi kama Mwokozi, watoto—kuanzia katika mwaka wanapofikisha miaka 8—wanaalikwa kuweka malengo ya kukua kiroho, kijamii, kimwili na kiakili (ona Luka 2:52).
Wanaweza kutumia Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo kwa Watoto ili kuweka na kurekodi malengo.
12.3
Uongozi wa Watoto katika Kata
12.3.1
Uaskofu
Wajibu muhimu zaidi kwa askofu ni kwa ajili ya kizazi kinachoinukia katika kata yake. Askofu anaweza kumpangia mshauri ili amsaidie katika wajibu wake huo kwa ajili ya Watoto. Askofu au mshauri aliyempangia anakutana mara kwa mara na rais wa Watoto.
Askofu na Washauri Wake mara kwa mara wanahudhuria darasa la Watoto.
12.3.2
Urais wa Watoto
Askofu anamwita na kumsimika mwanamke mtu mzima kuhudumu kama rais wa Watoto katika kata.
Katika kitengo kidogo, rais wa Watoto anaweza kuwa kiongozi pekee aliyeitwa katika kikundi cha Watoto. Katika hali kama hii, anafanya kazi na wazazi kupanga masomo, muda wa kuimba na shughuli. Kama kitengo ni kikubwa vya kutosha, miito ya ziada inaweza kujazwa katika utaratibu huu: washauri, kiongozi wa muziki, walimu na viongozi wa darasa la watoto wadogo, katibu, na viongozi wa shughuli.
Urais wa Watoto unawasaidia wazazi wawaandae watoto kuingia na kuendelea kwenye njia ya agano.
Ili kukamilisha hili rais wa Watoto anaweza kumpangia mshiriki wa urais awasaidie wazazi wawaandae watoto wao kubatizwa na kuthibitishwa. Rais wa Watoto anaweza kumpangia mshiriki mwingine wa urais kuwasaidia wazazi kwenye maandalizi ya hekaluni na ukuhani kwa ajili ya watoto wao.
Rais wa Watoto ana majukumu ya ziada yafuatayo. Washauri wake wanamsaidia.
-
Kuhudumu kwenye baraza la kata.
-
Mara kwa mara kufanya mikutano ya urais wa Watoto na kukutana na askofu au mshauri wake aliyepewa jukumu.
-
Kusaidia kupanga huduma za ubatizo kwa watoto wa kumbukumbu wakati atakapoombwa kufanya hivyo (ona 18.7.2).
-
Kupanga na kuendesha ufunguzi wa mikutano ya Watoto ya Jumapili.
-
Kumhudumia kila mtoto binafsi, walimu, na viongozi katika darasa la Watoto.
-
Kuwafundisha viongozi wa Watoto na walimu wajibu wao na kuwasaidia katika wajibu huo kwa kuwatambulisha kwenye miito yao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 38).
-
Kusimamia kumbukumbu, ripoti, bajeti na fedha za Watoto.
12.3.4
Kiongozi wa Muziki na Mpiga Kinanda
Kiongozi wa muziki na mpiga kinanda wanawafundisha watoto injili ya Yesu Kristo kupitia muziki wakati wa muda wa kuimba.
Kama mpiga kinanda hayupo au kinanda hakipo, viongozi wanaweza kutumia muziki uliorekodiwa.
12.3.5
Walimu na Viongozi wa Watoto Wadogo sana
Urais wa Watoto hupendekeza kwa uaskofu wanaume na wanawake wa kuhudumu kama walimu wa Watoto. Waumini hawa wanaitwa kufundisha na kuhudumia kundi la watoto wenye umri maalumu.
Walimu wa Watoto hufundisha kutoka Njoo, Unifuate (umri wa miaka 3–11).
Viongozi wa watoto wadogo sana wanafundisha kutoka kwenye Tazama Watoto Wako Wadogo.
12.3.6
Viongozi wa Shughuli
Viongozi wa shughuli za Watoto wanawahudumia watoto pale wanapopanga huduma na shughuli kuanzia Januari ya mwaka watoto hao wanapofikisha umri wa miaka 8 (ona 12.2.1.3). Huduma na shughuli vinafokasi kwenye kazi ya wokovu na kuinuliwa. Ni za kuleta burudani na ni jumuishi.
12.5
Miongozo ya Ziada na Sera
12.5.1
Kuwalinda Watoto
Wakati watu wazima wanapochangamana na watoto katika mipangilo ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo.
Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org).