“Ni Ushindi Gani Huja Kwa Sababu ya Ufufuko?,” Liahona, 2023.
Njoo, Unifuate
1 Wakorintho 15
Ni Ushindi Gani Huja Kwa Sababu ya Ufufuko?
Mtume Paulo aliwafundisha Wakorintho mwili uliofufuka ulikuwa vipi. Miili yetu “hufufuliwa katika kutokuharibika … katika fahari … [na] katika nguvu” (1 Wakorintho 15:42–43). Alifundisha pia kwamba “mauti imemezwa kwa kushinda” (1 Wakorintho 15:54) lakini ushindi huu ni nini? Nukuu zifuatazo zinaweza kutusaidia tuelewe ushindi unaopatikana kwa sababu ya Ufufuko.