2010–2019
Mchungaji Mwema, Mwanakondoo wa Mungu
Mkutano Mkuu wa Aprili 2019


15:19

Mchungaji Mwema, Mwanakondoo wa Mungu

Yesu Kristo anatuita kwa sauti Yake na kwa jina Lake. Anatutafuta na kutukusanya. Anatufundisha jinsi ya kuhudumia kwa upendo.

Wapenda akina kaka na dada zangu, je, mmewahi wakati wowote kuwa na matatizo ya kukosa usingizi na kujaribu kuhesabu kondoo wa kufikirika? Wakati kondoo mwenye manyoya mengi akiruka uzio, unahesabu: 1, 2, 3, … 245, 246, … 657, 658,…1

Katika swala langu, kuhesabu kondoo kunanifanya nikose usingizi. Nina wasiwasi kumkosa au kumpoteza mmoja, na hilo linanifanya nikose usingizi.

Pamoja na kijana mchunga kondoo ambaye alikuja kuwa mfalme, tunatangaza:

“Bwana ndiye mchungaji wangu; sitapungukiwa na kitu.

“Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza.

“Hunihuisha nafsi yangu.”2

Kioo cha Mchungaji Mwema kilichotiwa doa

Katika majira haya ya Pasaka, tunasherehekea kwa ajili ya mchungaji mwema, ambaye pia ni Mwanakonoo wa Mungu. Katika majina Yake yote matakatifu, hakuna mengine ambayo ni mema au yenye nguvu. Tunajifunza mengi kutokana na marejeleo ya Mwokozi wetu juu Yake kama Mchungaji mwema na kutoka katika shuhuda za kinabii juu Yake kama Mwanakondoo wa Mungu. Majukumu haya na Alama hizi zinasaidizana kikamilifu—Je ni nani ambaye yu bora kumsaidia kila mwanakondoo kuliko mchungaji Mwema, na ambaye anafaa zaidi kuwa Mchungaji wetu mwema kuliko Mwanakondoo wa Mungu?

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye wa pekee”, na Mwana pekee wa Mungu alitoa maisha Yake kwa utii bila kusita kwa Baba Yake.3 Yesu anashuhudia, “Mimi ndimi mchungaji mwema: mchungaji mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo.”4 Yesu alikuwa na uwezo wa kutoa maisha Yake na uwezo wa kuyatwaa tena.5 Pamoja na Baba Yake, Mwokozi wetu kwa kipekee anatubariki, vyote kama mchungaji wetu mwema na kama Mwana kondoo wa Mungu.

Kama Mchungaji wetu Mwema,Yesu Kristo anatuita kwa sauti Yake na kwa jina Lake. . Anatutafuta na kutukusanya. Anatufundisha jinsi ya kuhudumia kwa upendo. Acha tufikirie dhamira hizi tatu, kuanzia na Yeye kutuita kwa sauti Yake na kwa jina Lake.

Kwanza, Mchungaji wetu mwema “huwaita kondoo wake kwa jina. … Wanaijua sauti Yake.”6 Na “katika jina lake mwenyewe anakuita, ambalo ni jina la Kristo.”7 Tunapotafuta kwa dhamira ya kweli kumfuata Yesu Kristo, msukumo wa kiungu huja katika kutenda mema, kumpenda Mungu, na kumtumikia Yeye.8 Tunapojifunza, kutafakari, na kusali; tunaporudia tena mara kwa mara maagano ya sakramenti na maagano ya hekaluni; na tunapowaalika wote waje kwenye injili Yake na ibada zake, tunasikiliza sauti Yake.

Katika siku yetu, Rais Russell M.Nelson anatushauri kuliita Kanisa la urejesho kwa jina alililofunua Yesu Kristo—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.9 Bwana alisema, “Chochote mtakacho fanya, mtakifanya katika jina langu; kwa hiyo mtaliita kanisa katika jina langu; na mtamlingana Baba katika jina langu ili aweze kubariki kanisa kwa ajili yangu.”10 Kote ulimwenguni, katika mioyo na nyumba zetu, tunamlingana Baba katika jina la Yesu Kristo. Tunashukrani kwa baraka ya ukarimu kama hii ya kuabudu kunakolenga nyumbani, kunakosaidiwa na Kanisa, mafunzo ya injili, na shughuli za kifamilia zenye siha.

Pili, Mchungaji wetu Mwema anatutafuta na kutukusanya kwenye zizi lake moja. Anauliza, “Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotelewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?”11

Mwokozi wetu anamfikia mmoja na kwa wale tisini na tisa, mara nyingi kwa wakati mmoja. Tunapohudumia, tunawatambua wale tisini na tisa ambao ni imara na thabiti, hata wakati tuna shauku ya kumpata yule mmoja ambaye amepotea. Bwana wetu hututafuta na kutuokoa kutoka sehemu zote,“12 kutoka pande nne za dunia.13 Anatukusanya kwa agano takatifu na damu Yake ya upatanisho.14

Mwokozi aliwaambia wafuasi wake wa Agano Jipya, “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili.”15 Katika Amerika, Bwana aliyefufuka alishuhudia kwa watoto wa agano wa Lehi, “Na ninyi ni kondoo wangu.”16 Na Yesu alisema bado kondoo wengine wangesikia sauti Yake.17 Ni baraka iliyoje kuwa na Kitabu cha Mormoni kama ushuhuda mwingine kushuhudia sauti ya Yesu Kristo!

Yesu Kristo analialika Kanisa kuwapokea wote wanao sikia sauti Yake18 na kutii amri zake. Mafundisho ya Kristo yanajumuisha ubatizo kwa maji na kwa moto na Roho Mtakatifu.19 Nefi anauliza, “Na sasa, kama Mwanakondoo wa Mungu, akiwa mtakatifu, alihitaji kubatizwa kwa maji, ili kutimiza utakatifu wote, Ee basi, jinsi gani tunahitaji zaidi sisi, tusio watakatifu, kubatizwa, ndio, hata kwa maji!”20

Yohana anambatiza Yesu

Leo, Mwokozi wetu anatamani kwamba kile tunachofanya na kile tunachookuwa kitawaalika wengine kuja, kumfuata Yeye. Njoo upate upendo, uponyaji, muunganiko, na agano ndani Yake, ikijumuisha ndani ya hekalu takatifu la Mungu, ambapo ibada takatifu za wokovu zinaweza kubariki wanafamilia wote, hivyo kukusanya Israel pande zote za pazia.21

Tatu, wakati “Kama Mchunga wa Israel,”22 Yesu Kristo anaonesha kwa mfano jinsi wachungaji katika Israel wanavyohudumia kwa upendo. Wakati Bwana wetu anapouliza kama tunampenda, kama alivyofanya na Simoni Petro, mwokozi wetu anaomba sana: “Lisha wanakondoo wangu. … Lisha Kondoo Wangu. … Lisha kondoo wangu.”23 Bwana anaahidi kwamba wakati wachungaji Wake wanapolisha kondoo na wana kondoo Wake, wale katika zizi Lake “hawata hofu tena, wala kufadahaika, wala kupungukiwa.”24

Mchungaji wetu mwema anatutahadharisha kwamba wachungaji katika Israeli hawapaswi kusinzia,25 wala kutawanyika au kusababisha kondoo kupotea,26 wala kutafuta njia zetu wenyewe kwa manufaa yetu wenyewe.27 Wachunga kondoo wa Mungu wanatakiwa kuimarisha, kuponya, kufunga kile kilicho vunjika, kuleta tena kile ambacho kilitupiliwa mbali, kutafuta kile ambacho kilipotea.28

Bwana pia anaonya juu ya wachungaji wenye manufaa binafsi, ambao “hawawajali kondoo,“29 na “manabii wa uongo ambao wanawajia katika ngozi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.“30

Mchugaji wetu mwema hufurahi wakati tunapotumia uhuru wetu binafsi wa kuchagua kwa dhamira na imani. Wale katika zizi lake wana mwangalia Mwokozi wetu kwa shukrani kwa sababu ya dhabihu Yake ya upatanisho. Tunafanya agano kumfuata Yeye, si kwa kukaa tu, si kwa kutokujua, au “kwa kuona aibu” lakini kwa kutamani kwa mioyo yetu yote na akili kumpenda Mungu na jirani yetu, tukibebeana mizigo na kufurahi katika shangwe za wenzetu. Kama Kristo kwa uhuru alivyotoa mapenzi yake kwa ajili ya mapenzi ya Baba, nasi pia kwa heshima kubwa tunajichukulia juu yetu jina Lake. Kwa shangwe tunatafuta kujiunga kwenye kazi Yake ya kukusanya na kuhudumia watoto wote wa Mungu.

Akina kaka na dada, Yesu Kristo ni Mchungaji wetu mkamilifu. Kwa sababu ametoa maisha Yake kwa ajili yetu, na kwa sasa kwa utukufu amefufuka, Yesu Kristo pia ni Mwanakondoo mkamilifu wa Mungu.31

Mwana kondoo wa dhabihu wa Mungu alingojewa toka mwanzo. Malaika alimwambia Adamu sadaka yake “ni mfano wa sadaka ya Mwana Pekee wa Baba,” ambayo hutualika “kutubu na kumlingana Mungu katika jina la Mwana milele yote.”32

Baba Ibrahimu, ambaye alianzisha baraka za agano kwa ajili ya mataifa yote ya dunia, alipata uzoefu wa nini ilimaanishwa kumtoa mwanae mpendwa.

“Na Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu: naye akasema, Mimi hapa mwanangu. Na akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo: lakini yuko wapi mwana-kondoo …?

“Na Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu.”33

Mitume na manabii waliona kabla na walishangilia katika huduma iliyotayarishwa tayari ya Mwanakondoo wa Mungu. Yohana katika Ulimwengu wa Kale na Nefi katika Ulimwengu Mpya walishuhudia juu ya “Mwanakondoo wa Mungu,”34 “naam, hata Mwana wa Baba wa milele[,] … Mkombozi wa ulimwengu.”35

Abinadi alishuhudia juu ya dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo: “Sisi sote, kama kondoo, tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake; na Bwana amejitwika [maovu] yetu sisi sote.“36 Alma aliita dhabihu kuu na ya mwisho ya Mwana wa Mungu “kitu kimoja ambacho ni muhimu kuliko vyote.” Alma alitia moyo, “Muwe na imani juu ya Mwanakondoo wa Mungu,” “njooni na msiogope.”37

Rafiki mpendwa alishiriki jinsi alivyopata ushuhuda wake wa thamani wa upatanisho wa Yesu Kristo. Alikua akiamini dhambi siku zote ilileta adhabu kubwa, inayobebwa na sisi peke yetu. Alimsihi Mungu ili kuelewa uwezekano wa msamaha mtakatifu. Aliomba ajue jinsi Yesu Kristo anavyoweza kuwasamehe wale wanaotubu, jinsi huruma inavyoweza kutosheleza sheria.

Siku moja sala yake ilijibiwa katika uzoefu wa kubadilisha wa kiroho. Kijana aliyekata tamaa alikuwa akitoka nje ya duka la chakula huku akikimbia akiwa amebeba vifurushi viwili vya chakula alivyoiba. Alikimbia kwenye mtaa wenye shughuli nyingi, akikimbizwa na meneja wa duka, ambaye alimkamata na kuanza kupiga yowe na kupigana. Badala ya hukumu kwa kijana aliyejawa hofu kama mwizi, rafiki yangu alijikuta bila kutegemea amejawa na huruma kubwa sana kwa ajili yake. Bila woga au kushugulika kwa ajili ya usalama wake mwenyewe, alitembea moja kwa moja kuwaelekea wanaume wawili waliokuwa wakipigana. Alijikuta akisema mwenyewe “Nitalipa hicho chakula. Tafadhali mwache aende. Tafadhali niache nilipie hicho chakula.”

Akishawishiwa na Roho Mtakatifu na kujazwa na upendo ambao kamwe hajawahi kuuhisi, rafiki yangu alisema, “Yote niliyotaka kufanya ilikuwa ni kumsaidia na kumwokoa kijana.” Rafiki yangu alisema alianza kumwelewa Yesu Kristo na Upatanisho Wake—jinsi gani na kwa nini pamoja na upendo wa kweli na mkamilifu kwa hiari yake angeweza kutoa dhabihu kuwa Mwokozi na Mkombozi wake, na kwa nini alimtaka Yeye awe hivyo.38

Ndio maana tunaimba:

Ona, Mchungaji Mwema anatafuta,

Anatafuta wanakondoo waliopotea,

Awarudisha kwa shangwe,

Wakiokolewa kwa gharama kama hiyo isiyo na mwisho.39

Kama Mwana kondoo wa Mungu, Mwokozi wetu anajua wakati tunapohisi upweke, kupungukiwa, mashaka, au woga. Katika ono, Nefi, aliona nguvu za Mwanakondoo wa Mungu, “[zikishuka] juu ya watakatifu wa kanisa la Mwanakondoo, na juu ya watu wa agano wa Bwana.” Ingawa “walitawanyika kote usoni mwa dunia; … na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu.”40

Ahadi hii ya matumaini na faraja inajumuisha siku yetu.

Je wewe ni muumuni pekee wa Kanisa katika familia yako, shule, mahali pa kazi, au jamii? Je Tawi lako wakati mwingine hujihisi dogo au limetengwa? Je umehamia kwenye sehemu mpya, pengine kwenye lugha au desturi usiyoifahamu? Pengine hali ya maisha yako imebadilika, na vitu ambavyo kamwe hukufikiria vinawezekana sasa vinakukabili? Mwokozi wetu anatuhakikishia, vyovyote tulivyo, kwa hali zozote tulizo nazo, katika maneno ya isaya: “Yeye atawakusanya wanakondoo kwa mkono wake, na kuwachukua kifuani mwake, na kwa ukarimu kuwaongoza wale ambao ni wadogo,”41

Mchungaji Mwema akikusanya kondoo Wake

Akina kaka na akina dada, mchungaji wetu Mwema anatuita kwa sauti yake na kwa jina Lake. Anatafuta, anakusanya, na anakuja kwa watu Wake. Kupitia nabii Wake anayeishi na kila mmoja wetu, anawaalika wote kupata amani, lengo, uponyaji, na furaha katika utimilifu wa injili Yake ya urejesho na kwenye njia Yake ya agano. Kupitia mfano, Anawafundisha wachungaji wa Israeli kuhudumia katika upendo Wake.

Kama Mwanakondoo wa Mungu, utumishi wake mtakatifu ulichaguliwa kabla na ulifurahiwa na mitume na manabii. Upatanisho wake, usio na mwisho na wa milele, ni kitovu kwenye mpango wa furaha na lengo la uumbaji. Anatuhakikishia kwamba anatubeba karibu na moyo Wake.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, hebu tutamani kuwa “wafuasi wanyenyekevu wa Mungu na Mwanakondoo,”42 pengine siku moja majina yetu yapate kuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha mwanakondoo,43 ili tuimbe wimbo wa Mwanakondoo,44 ili tualikwe kwenye chukula cha jioni cha Mwanakondoo.45

Kama Mchungaji na Mwanakondoo, Anaita: njoo tena “kwenye elimu ya kweli … ya Mkombozi [wako], …mchungaji [wako] mkuu na wa kweli.”46 Anaahidi kwamba “kwa rehema yake [sisi] tunaweza [kuwa] wakamilifu katika Kristo.”47

Wakati huu wa majira ya Pasaka, tunamsifu Yeye:

“Mwenye kustahili sifa ni Mwanakondoo!”48

“Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo!“49

Ninashuhudia juu Yake, Mchungaji wetu Mkamilifu, Mwanakondoo mkamilifu wa Mungu. Anatuita kwa jina letu, katika jina Lake—hata jina takatifu na tukufu la Yesu Kristo—amina.

Muhtasari

  1. Wimbo maarufu unapendekeza:

    Ninapokuwa na hofu na kutoweza kulala,

    Ninahesabu baraka zangu badala ya kondoo.

    Na ninasinzia nikihesabu baraka zangu.

    (Irving Berlin, “Hesabu Baraka Zako Badala ya Kondoo” [1952])

  2. Zaburi 23:1–3.

  3. Yohana 3:16.

  4. Yohana 10:11.

  5. Ona Yohana 10:15, 17–18.

  6. Yohana 10:3–4.

  7. Alma 5:38; ona pia Alma 5:37, 39, 59–60.

  8. Ona Moroni 7:13; Mafundisho na Maagano 8:2–3.

  9. Ona Russell M. Nelson, “Jina Sahihi la Kanisa,” Liahona Nov. 2018, 87–89.

  10. 3 Nefi 27:7; mkazo umeongezwa.

  11. Luka 15:4; msisitizo umeongezwa; ona pia Mafundisho na Maagano 18:15.

  12. OnaEzekiel 34:12; ona pia Yeremia 31:10; Ezekieli 34:6, 11–14; Mika 5:8; Mathayo 10:6; 15:24. Tabiri hizi za kutawanyika na tabiri na ahadi za agano la kukusanyika ni mada endelevu ya manabii, ikimjumuisha Rais Russell M. Nelson

  13. 1 Nefi 22:25.

  14. Ona Waebrania 13:20.

  15. Yohana 10:16; Ona pia 3 Nefi 15:21; 16:1, 3; Mafundisho na Maagano 10:59 –60

  16. 3 Nefi 15:24; ona pia 3 Nefi 15:17, 21.

  17. Ona 3 Nefi 16:1, 3; ona pia Mafundisho na Maagano 10:59–60.

  18. Ona Mosia 26:21.

  19. Ona 2 Nefi 31:13–14, 21.

  20. 2 Nefi 31:5; ona pia Alma 7:14

  21. Ona Malaki 4:5–6; Yohana 15:9–13; Mosia 25:18; Helamani 11:21; ona pia Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli” (ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018), HopeofIsrael.ChurchofJesusChrist.org; Russell M. Nelson, “Kukusanyika kwa Israeli Iliyotawanyika,” Liahona, Nov. 2006, 79–82.

  22. Zaburi 80:1

  23. Yohana 21:15–17; ona pia sura nzima.

  24. Yeremia 23:4

  25. Ona Nahumu 3:18.

  26. Ona Yeremia 23:1; 50:6, 44.

  27. Ona Isaya 56:11; Ezekieli 34:2–6

  28. Ona Ezekieli 34:2–6.

  29. Yohana 10:13.

  30. 3 Nefi 14:15; ona pia Mathayo 7:15; Alma 5:60

  31. Ona 2 Nefi 9:10–12. Kwa kushinda kifo cha mwili na utengano wa kiroho, Mwanakondoo wa Mungu anawezesha mkusanyiko wa vyote kwa hiyo kuna, katika muda na milele, Mchungaji mmoja.

  32. Musa 5:7–8

  33. Mwanzo 22:7–8; na pia Yakobo 4:5.

  34. Yohana 1:29; 1 Nefi 11:21

  35. 1 Nefi 11:21, 27.

  36. Mosia 14:6; ona pia Isaya 53:6.

  37. Alma 7:7, 14–15.

  38. Mazungumzo na Pornthip “Tippy” Coyle, Feb. 2019, imetumika kwa ruhusa.

  39. “Dear to the Heart of the Shepherd,” Nyimbo za Kanisa, na. 221. Nyimbo zingine ambazo zinampa umuhimu Mchungaji wetu na kondoo Wake zinajumuisha zifuatazo: “The Lord My Pasture Will Prepare,” Nyimbo za Kanisa, na 109:

    Bwana malisho yangu ataandaa

    Na kunilisha kwa uangalizi wa Mchungaji.

    Uwepo Wake utakidhi hitaji langu,

    Na kunilinda kwa jicho la uangalizi.

    Nyendo zangu za mchana atazilinda

    Na masaa yangu tulivu ya usiku atayalinda.

    “Help Me Teach with Inspiration,” Nyimbo za Kanisa, na. 281:

    Nisaidie kuwapata wanakondoo wako wanaotangatanga;

    Nisaidie kuwaleta kwenye ulinzi wako.

    Nifundishe, Bwana, kuwa Mchungaji;

    Baba, nisaidie kuwalisha kondoo wako.

    “Come, All Ye Sons of God,” Nyimbo za Kanisa, na. 322:

    Kazi ya siku za mwisho imeanza,

    Kuwaleta pamoja Israeli iliyotawanyika,

    Na kuwarejesha Sayuni ili wamsifu Mwanakondoo.

    Njooni, enyi kondoo wote mliotawanyika, na msikilizeni Mchungaji wenu.

  40. 1 Nefi 14:14; ona pia 1 Nefi 13:35,37:”dhahiri na ya thamani [maandiko yata]… kuja kutoka leo na kuendelea…kwa karama na nguvu za Mwanakondoo. … Kama [sisi] tutavumilia mpaka mwisho … [sisi] tutaokolewa katika ufalme usio na mwisho wa Mwanakondoo.”

  41. Isaya 40:11.

  42. Helamani 6:5:

  43. Ona Ufunuo 21:27.

  44. Ona Ufunuo 15:3; Mafundisho na Maagano 133:56.

  45. Ona Ufunuo 19:9, Mafundisho na Maagano 58:11; ona pia Ufunuo 7:17: “Kwa kuwa Mwanakondoo … atawalisha, na atawaongoza kwenye chemichemi ya maji ya uzima: na Mungu atawafuta machozi yao yote kutoka machoni mwao”; Ufunuo 22:1: “Mto safi wa maji ya uzima safi kama fuwele, yakitoka kutoka kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo.”

  46. Helamani 15:13

  47. Ona Moroni 10:32–33.

  48. Ufunuo 5:12.

  49. Mafundisho na Maagano 109:79.