Ujumbe wa kila Mwezi katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Desemba 2025
Tunajua nini kuhusu wachungaji katika Krismasi ya kwanza?
Wachungaji, na Brian Call
Tunajua mambo machache kuhusu wachungaji katika Krismasi ya kwanza.
Walikuwa karibu na Bethlehemu. Wachungaji walikuwa “katika nchi ile ile” ambapo kuzaliwa kwa Kristo kulitokea (Luka 2:8). Na waliweza kufika Bethlehemu kwa miguu wakati Alipokuwa bado yuko pale (ona Luka 2:15–16).
Walikuwa wakifanya wajibu wao. Wachungaji hawa walikuwa “wakikaa makondenii, wakilinda kundi lao kwa zamu usiku” (Luka 2:8). Walikuwa wachungaji wema na waaminifu, kama Mwokozi—alivyo Mchungaji Mwema (ona Yohana 10:11, 14).
Walijua unabii juu ya Masiya. Inavyonekana walijua malaika alikuwa akizungumzia nini wakati alipotangaza kuzaliwa kwa “Kristo Bwana” (Luka 2:11), Masiya aliyetolewa unabii tangu kale.
Walikuwa na ari kubwa. Wakati malaika alipowaambia kuhusu “mtoto mchanga … amelala katika hori la kulia ng’ombe” (Luka 2:12), wakaenda “kwa haraka” kumwona (Luka 2:16).
Walishiriki ile habari njema. “Walitoa habari” ya kile walichokuwa wamesikia na kuona kuhusu ujumbe wa malaika juu ya kuzaliwa kwa Kristo (Luka 2:17).
Walimshukuru na kumsifu Mungu. Baada ya haya yote, “walirudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu Mungu kwa mambo yote waliyoyasikia na kuyaona” (Luka 2:20).
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, December 2025. Swahili. 19617 743