2025
Watakatifu Wanaenda Magharibi
Rafiki la Desemba 2025


“Watakatifu Wanaenda Magharibi,” Rafiki, Desemba 2025, 26–28.

Ujumbe wa kila mwezi katika Rafiki, Desemba 2025

Watakatifu Wanaenda Magharibi

Brigham Young akiangalia wakati watu wakifanya kazi kwenye Hekalu la Nauvoo ambalo halijaisha.

Baada ya kifo cha Joseph Smith, Brigham Young na Mitume wengine waliliongoza Kanisa. Brigham alijua Watakatifu walipaswa kuondoka Nauvoo kwa sababu hapakuwa salama. Lakini Bwana aliwataka wamalizie kujenga hekalu kwanza.

Brigham Young akiwakaribisha watu hekaluni

Wakati hekalu lilipokuwa tayari, maelfu ya Watakatifu walifanya maagano na Bwana na waliunganishwa kama familia.

Watakatifu wakitembea kupita kwenye dhoruba ya theluji

Sasa ilikuwa ni wakati wa kuanza safari yao kuelekea magharibi. Hali ya hewa ilikuwa baridi, na watu walikuwa wagonjwa na wenye njaa.

Familia zikiwasaidia wengine kupata chakula na mablanketi katika baridi

Brigham alisali kwa ajili ya msaada. Bwana alisema wanapaswa kusaidiana, na Yeye angewabariki na kuwasaidia.

Familia ikiwa imepiga magoti kando ya kaburi

Safari bado ilikuwa ngumu sana. Baadhi ya watu walifariki. Lakini kwa sababu ya maagano yao ya hekaluni, Watakatifu walijua wangewaona wanafamilia wao tena.

Brigham Young akiwa katika mkokoteni akiliangalia Bonde la Salt Lake

Watakatifu wa kwanza waliwasili katika Bonde la Salt Lake mwaka 1847. Hapa wangeweza kumwabudu Bwana na kuifanya kazi Yake kwa amani.

Picha za mahekalu na wamisionari pamoja na ramani ya ulimwengu katika upande wa nyuma

Kwa miaka mingi, Watakatifu zaidi walifika na kujenga mahekalu zaidi. Wamisionari walisafiri ulimwenguni kote kuifundisha injili ya Yesu Kristo. Kanisa la Mwokozi liliendelea kukua, likiwabariki watoto wa Baba wa Mbinguni kila mahali.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Yeye Ni Nuru, Uzima, na Tumaini la Ulimwengu

Ukurasa PDF wa kupaka rangi wa mtoto Yesu akiwa horini na mwana kondoo

Kielelezo na Corey Egbert

Je, wewe unafanya nini wakati wa Krismasi ili kumkumbuka Yesu Kristo?