"Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo," Rafiki, Oktoba 2025, 26–28.
Ujumbe wa kila mwezi wa Rafiki, Oktoba 2025
Jane Manning Anasafiri kwenda Nauvoo
Mahali ambapo Jane Manning aliishi, baadhi ya watu walimtendea vibaya kwa sababu ya rangi yake ya ngozi. Siku moja, alisikia mafundisho ya wamisionari. Punde alibatizwa.
Familia ya Jane pia ilibatizwa. Wote walitaka kuwa pamoja na Watakatifu huko Nauvoo. Kwa hiyo walianza safari yao.
Familia ya Jane ilitaka sehemu ya safari kutumia mashua, lakini hawakuwa na fedha za kutosha. Kwa hivyo iliwabidi watembee maili 800 (kilometa 1,300).
Iliwabidi kuvuka kijito chenye kina kirefu na kulala nje kwenye baridi. Lakini walidhamiria kufika Nauvoo. Walijitia moyo kwa kuimba walipokuwa wakitembea.
Familia ya Jane ilitembea mpaka viatu vyao vikachakaa na miguu yao kuumia. Lakini walipomwomba Mungu kwa ajili ya msaada, Yeye aliiponya miguu yao.
Waliwasaidia watu waliokutana nao njiani. Walisaidia hata kumponya mtoto mgonjwa kwa sababu ya imani yao.
Hatimaye, Jane na familia yake walifika Nauvoo! Wakati Joseph Smith aliposikia yote waliyokuwa wamepitia, alimwambia Jane, "Mungu akubariki. Nyinyi sasa mpo miongoni mwa marafiki."
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Yesu Ananitaka Nimpende Kila Mtu
Kielelezo na Corey Egbert
Unaonyeshaje upendo kwa wengine?
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/19. Tafsiri iliidhinishwa: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, October 2025. Swahili. 19630 000