“Kupokea Sakramenti,” Rafiki, Agosti 2023, 33.
Kupokea Sakramenti
Vielelezo na Barbara Bongini
Kila wiki, tunapokea sakramenti. Inatusaidia tumkumbuke Yesu Kristo na ahadi ya kumfuata Yeye.
Kabla ya kupokea sakramenti, mimi ninaweza …
-
Kuimba wimbo wa dini
-
Kutazama mkate na maji vikiandaliwa
-
Kusikiliza sala za sakramenti
Wakati wa sakramenti, ninaweza …
-
Kupokea mkate na maji kwa staha
-
Kufikiria kuhusu kile Yesu alchokifanya kwa ajili yangu na kiasi gani Yeye ananipenda
-
Kukumbuka agano langu la ubatizo
Baada ya sakramenti, ninaweza kumkumbuka na kumfuata Yesu wiki yote kwa . . .
-
Kushika Amri Zake
-
Kuwa mkarimu kwa wengine
-
Kufuata msukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu
-
Kujiuliza mwenyewe, “Je, Yesu angefanya nini?”