Kuwaimarisha Waumini Wapya
Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi


“Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi (2020)

“Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi,” Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi

Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi: Muhtasari Uliopendekezwa wa Mafunzo

Waumini na wamisionari wana jukumu muhimu katika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kuendelea kwenye njia ya agano. Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kwa juhudi za kila siku za umisionari katika kata, ikiwa ni pamoja na kuwalea waumini wapya na wanaorudi. Chini ya maelekezo ya rais wa kigingi na askofu, marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kuhakikisha kwamba viongozi wa kata na akina kaka na akina dada wahudumiaji wanapokea na kutendea kazi maelekezo yafuatayo.

Kwa waumini wapya na wanaorudi kuweza kubakia kwenye njia ya agano, ni muhimu kwao (1) kuhisi kuwa wanastahili kupitia mahusiano yaliyoimarishwa kwa Mungu na waumini wengine, (2) kuamini katika Yesu Kristo na kuimarisha imani yao Kwake, na ( 3) kuwa wanafunzi wa Kristo kupitia uzoefu muhimu.

Shughuli zifuatazo zitakusaidia uwafundishe waumini wengine jinsi ya kutumia rasilimali muhimu ili kusaidia katika juhudi hii. Shughuli hizi zinaweza kukamilishwa katika mazingira ya baraza la kigingi au kata wakiwepo wamisionari wa muda wote. Sehemu mbili za mwanzo zinapaswa pia kutolewa kwa wenzi wa kuhudumu waliopangwa kwa waumini wapya na wanaorudi.

Chati: Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubaki kwenye Njia ya Agano

  1. Fungua Maktaba ya Injili (aplikesheni au ukurasa wa wavuti) na nenda kwenye Vitabu vya Maelezo na Miito, kisha Miito ya Kata au Tawi, na kisha Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi. (Nyenzo utakazohitaji kwa ajili ya mafunzo haya zinapatikana katika sehemu hii.) Fungua na upitie “Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubaki kwenye Njia ya Agano.” Kama mtu na mwenzake au kikundi, jadilini:

    • Kwa nini uzoefu huu ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia watu kuingia na kubaki kwenye njia ya agano?

  2. Tazama vipande vya video “The Bush Family Story” (katika sehemu ya Video za Kuwamarisha Waumini Wapya) au “The Battina and Sydney Story” na “The Lynette and Sean Story” (katika sehemu ya Video za Kuwaimarisha Waumini Wanaorudi). Unapotazama video, tafuta jinsi ambavyo vitu vilivyo kwenye chati chini ya “Kabla ya Ubatizo au Kurudi Kanisani,” “Punde baada ya Ubatizo au Kurudi Kanisani,” na “Ndani ya Mwaka Wa Kwanza” vilitumika katika kila hadithi.

    7:12
    6:44

    Jadilini:

    • Ni kipi tunafanya vyema zaidi kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi ili wasonge mbele?

    • Ni eneo lipi moja au mawili tunahisi tunaweza kujiboresha?

  3. Tazama kipande cha video “Umuhimu wa Urafiki.” Jadilini:

    • Kwa nini kuwa na urafiki wa kweli na waumini ni moja ya sababu imara zaidi katika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kuingia na kubaki kwenye njia ya agano?

    • Tunawezaje kusaidia kujenga urafiki wa kweli mapema iwezekanavyo? Tunawezaje kudumisha urafiki huu?

  4. Tazama kipande cha video “Kufanya kazi Pamoja.” Jadilini:

    • Je, waumini na wamisionari walifanyaje kazi pamoja ili kukidhi mahitaji ya familia ya Bush?

    • Ni kipi kingeweza kuboreshwa katika kitengo chetu ili waumini na wamisionari wafanye kazi pamoja kwa ufanisi zaidi katika juhudi hizi?

  5. Tazama kipande cha video “Kuwabariki Waumini Wapya na Wanaorudi Kupitia Mabaraza.”

    5:25

    Jadilini:

    • Ni kwa jinsi gani uaskofu, baraza la kata, na mikutano ya uratibu ya wamisionari ilifanya kazi kwa umoja katika kusaidia maendeleo ya Salvador?

    • Ni kwa jinsi gani nyenzo ya Maendeleo kwenye Njia ya Agano iliwasaidia viongozi?

    • Nini kinaweza kuboreshwa katika kitengo chetu ili mabaraza na mikutano hii ikidhi vyema mahitaji ya waumini wapya na wanaorudi?

Njia Yangu ya Agano

  1. Katika kipengele hicho hicho kwenye Kuwaimarisha Waumini Wapya na Wanaorudi katika Maktaba ya Injili, fungua Njia Yangu ya Agano na kisha nenda “Njia yangu ya Agano” utangulizi. Someni ukurasa huu pamoja na mjadili jinsi gani Njia yangu ya Agano ingeweza kutumika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi. Pitieni angalau uzoefu wa aina mbili ndani ya Njia Yangu ya Agano. Jadilini:

    • Ni jinsi gani akina kaka na akina dada wahudumiaji wanafanya kazi pamoja kuwasaidia waumini wapya au wanaorudi?

    • Ni kwa jinsi gani uzoefu huu unaweza kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kujifunza injili, kumhisi Roho, na kujenga urafiki wa kudumu na waumini wengine?

  2. Panga jinsi utakavyowasaidia waumini wapya na wanaorudi unaowahudumia ili wafikie Njia Yangu ya Agano. Ikiwa wanatumia kifaa cha Android, wanaweza kupakua app ya Maktaba ya Injili kutoka Google Play store hapa. Ikiwa wanatumia kifaa cha iOS, wanaweza kupakua app ya Maktaba ya Injili kutoka Apple App Store hapa. Unaweza pia kutoa nakala iliyochapishwa. (Kumbuka: Waumini wapya na wanaorudi wanaweza kupata Njia Yangu ya Agano kwa kwenda Watu Wazima na kisha Waumini Wapya au Wanaorudi katika Maktaba ya Injili.)

Maendeleo kwenye Njia ya Agano

Ripoti ya Maendeleo kwenye Njia ya Agano inatumika kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kufuatilia maendeleo yao kwenye njia ya agano wakati wa miaka yao miwili ya kwanza ya uumini wa Kanisa au kurudi kwenye shughuli za Kanisa. Pia inatumika kuwasaidia watu wanaofundishwa na wamisionari. Inapatikana kwa viongozi wa eneo husika kupitia menyu ya Ripoti katika app ya Zana za Muumini na LCR (Rasilimali za Kiongozi na Karani).

Ripoti ya Maendeleo kwenye Njia ya Agano imejumuishwa na app ya Hubiri Injili Yangu ambayo wamisionari wanaitumia. Wakati taarifa inaposasishwa katika mojawapo ya hizo, nyingine inasasishwa kiautomatiki. Ripoti inapaswa kutumika kama chombo muhimu cha uratibu na viongozi wa eneo husika. Wanapaswa kuifungua na kuipitia mara kwa mara, ikijumuisha kama sehemu ya mikutano ya baraza la kata, mikutano ya uratibu, na wakati wanapokutana na wamisionari.

Viongozi wafuatao wanaweza kufikia na kusasisha maendeleo ya muumini mpya au anayerudi kupitia Maendeleo kwenye Njia ya Agano:

  • Muumini mpya (ikijumuisha wazazi wa watoto)

  • Uaskofu( ikijumuisha makarani na makatibu)

  • Urais wa akidi ya wazee (ikijumuisha makatibu)

  • Urais wa Muungano wa Usaidizi (ikijumuisha makatibu)

  • Kiongozi wa misioni wa kata (ikijumuisha kiongozi msaidizi wa misioni wa kata)

  • Wamisionari wa kata

  1. Ili kufikia ripoti, fungua app ya Zana za Muumini (au Rasilimali za Kiongozi na Karani [LCR] mtandaoni), nenda kwenye Ripoti, na kisha chagua Maendeleo kwenye Njia ya Agano. Utakuwa na uchaguzi wa kuchagua mojawapo ya vipengele vitatu: Waumini Wapya, Wanaorudi, na Wanaofundishwa. Kila kipengele kinaonesha taarifa za msingi kuhusu wale ambao wamebatizwa ndani ya miaka miwili iliyopita na wanaishi katika kitengo chako na wale ambao kwa sasa wanafundishwa na wamisionari. Wakati wanapotazama kipengele cha Waumini Wanaorudi, viongozi wafuatao wana fursa ya kumwongeza muumini anayerudi baada ya kupokea ruhusa kutoka kwa muumini anayerudi kwamba waongezwe:

    • Uaskofu( ikijumuisha makarani na makatibu)

    • Urais wa Akidi ya Wazee

    • Urais wa Muungano wa Usaidizi

    • Kiongozi wa misioni wa kata (ikijumuisha kiongozi msaidizi wa misioni wa kata)

    Pitieni orodha ya waumini wapya na wanaorudi na jadilini jinsi wanavyoendelea.

  2. Chagua jina la muumini mpya au anayerudi (au chagua Angalia Maelezo katika LCR na IOS). Maelezo ya ziada juu ya maendeleo ya mtu huonyeshwa. Jadilini:

    • Kuna uhusiano gani kati ya taarifa hii na Njia Yangu ya Agano?

    • Ni kipi kinahitajika kutokea ili kumsaidia kila mmoja wa waumini wetu wapya kupiga hatua?

  3. Wale walio na ufikiaji wa kuhariri wanaweza:

    • Kurekodi mahudhurio ya mkutano wa sakramenti. (Kumbuka: Ikiwa muumini mpya au anayerudi hawezi kuhudhuria mkutano wa sakramenti kwa sababu za kiafya, waweke kama wahudhuriaji ikiwa muumini mpya ameweza kupokea sakramenti nyumbani au anahudhuria mkutano wa sakramenti akiwa mbali.)

    • Ongeza jina la rafiki kwenye taarifa ya muumini mpya au anayerudi.

    • Sasisha kanuni zilizofundishwa (masomo ya umisionari baada ya ubatizo).

    • Hakikisha taarifa kuhusu akina kaka na akina dada wahudumiaji ni sahihi.

  4. Arafa za ndani ya app zitaonekana wakati Maendeleo ya mtu kwenye Njia ya Agano yanapopendekeza ushiriki mdogo katika shughuli za Kanisa.

  5. Waumini wapya na wanaorudi wanaweza pia kusasisha maendeleo yao wenyewe. Waruhusu waumini wapya wafuatilie taarifa zao binafsi kutoka kwenye kielekezo katika Nyenzo za Muumini. Kisha, mruhusu muumini abofye kwenye Maendeleo kwenye Njia ya Agano.

  6. Marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanawajibika kuhakikisha taarifa ya muumini mpya imesasishwa kwa wakati sahihi. Wanaweza kunaibisha jukumu hili. Jadilini kuhusu nani atasasisha taarifa ya muumini mpya, mara ngapi (inapendekezwa angalau kila wiki), na ni jinsi gani Maendeleo kwenye Njia ya Agano yatatumika kwenye baraza la kata na mikutano ya uratibu ya kila wiki.

Hitimisho

  1. Onesha kipande cha video “Jinsi Mahekalu na Historia ya Familia Vinavyowaimarisha Waumini Wapya.”

    5:13

    Jadilini jinsi juhudi zenu zinavyoweza kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kubaki kwenye njia ya agano (ona Yohana 15:16) na hatimaye kupokea ibada zote za wokovu na kuinuliwa. Panga kile ambacho kitengo chako kitafanya ili kuwalea waumini wapya na wanaorudi pamoja na wale wanaofundishwa na wamisionari katika mkusanyiko wako.