Maswali ya Usaili kwa Wamisionari Watarajiwa
Maaskofu na marais wa vigingi wanaalikwa “kufanya usaili wa kina, wa kutafiti kiroho, na wenye kuinua” na kila anayetaka kuwa mmisionari kwa kutumia maswali yafuatayo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 24.4.2).
-
Je, una imani na ushuhuda juu ya Mungu, Baba wa Milele; Mwanaye, Yesu Kristo; na Roho Mtakatifu?
-
Je, una ushuhuda juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo na wa jukumu Lake kama Mwokozi na Mkombozi wako?
Tafadhali shiriki nami ushuhuda wako. Ni kwa jinsi gani Upatanisho wa Yesu Kristo umeathiri maisha yako?
-
Je, una ushuhuda wa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo na ukweli wa Kitabu cha Mormoni?
Ni kwa jinsi gani uelewa wako wa injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo na kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni vimekuza uhusiano wako na Yesu Kristo?
-
Je, unamkubali Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kama nabii, mwonaji na mfunuzi na kama mtu pekee duniani aliyepewa mamlaka ya kutumia funguo zote za ukuhani?
Je, unawakubali washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi?
Je, unawakubali Viongozi Wakuu wengine wenye Mamlaka na viongozi wa Kanisa wa eneo lako?
-
Bwana amesema kwamba mambo yote lazima “yafanyike katika usafi” mbele Yake (Mafundisho na Maagano 42:41).
Kwa nini kujitahidi kuwa msafi mbele za Mungu inajumuisha kuepuka ponografia?
Kutokana na uelewa wako, ina maana gani kuishi sheria ya usafi wa kimwili?
Je, unajitahidi kwa usafi wa kimaadili katika mawazo na tabia zako?
Je, unatii sheria ya usafi wa kimwili?
-
Je, unafuata mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo katika matendo yako ya siri na ya hadharani kwa wanafamilia yako na watu wengine?
-
Je, unaunga mkono au kudhamini mafundisho yoyote, matendo au kanuni zilizo kinyume na zile za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho?
-
Je, unajitahidi kuitakasa siku ya Sabato, kote nyumbani na kanisani; kuhudhuria mikutano yako; kujiandaa na kupokea sakramenti kwa kustahili; na kuishi maisha yako sawa sawa na sheria na amri za injili?
-
Je, unajitahidi kuwa mwaminifu katika yote unayoyafanya?
-
Je, wewe ni mlipa zaka kamili?
-
Kutokana na uelewa wako, ina maana gani kuishi Neno la Hekima?
Je, unatii Neno la Hekima?
-
Kama mmisionari, je, utaishi kulingana na viwango hivi tulivyovijadili?
-
(Swali hili huondolewa wakati wa kumfanyia usaili muumini ambaye hajapokea endaumenti.) Je unatii maagano uliyoyafanya hekaluni?
-
(Swali hili huondolewa wakati wa kumfanyia usaili muumini ambaye hajapokea endaumenti.) Je, unaheshimu fursa yako takatifu ya kuvaa gamenti jinsi ilivyoelekezwa kwenye ibada za mwanzo? (Soma maelezo ya “Uvaaji wa Gamenti ya Hekaluni”, yaliyojumuishwa hapa chini, kwa kila muumini).
-
Kutubu ina maana gani kwako, ikijumuisha kuungama dhambi zinazohitaji toba ya muda mrefu kwa usaidizi wa viongozi wa Kanisa, kwa mamlaka za ukuhani?
Je, kuna dhambi zinazohitaji toba ya muda mrefu kwa usaidizi wa viongozi wa Kanisa katika maisha yako ambazo zinahitaji kushughulikiwa na mamlaka za ukuhani kama sehemu ya toba yako?
-
Je, unajiona mwenye kustahili kumwakilisha Yesu Kristo na Kanisa Lake lililorejeshwa kama mmisionari?
Uvaaji wa Gamenti ya Hekaluni
“Gamenti ya ukuhani mtakatifu inatukumbusha juu ya pazia katika hekalu, na pazia hilo ni ishara ya Yesu Kristo. Unapovaa gamenti yako, unavaa alama takatifu ya Yesu Kristo. Kuivaa ni dhihirisho la nje la msimamo wako wa ndani wa kumfuata Yeye. Gamenti pia ni ukumbusho wa maagano yako ya hekaluni. Unapaswa kuvaa gamenti mchana na usiku katika maisha yako yote. Inapokuwa lazima iondolewe kwa ajili ya shughuli ambazo haziwezi kufanywa gamenti ikiwa imevaliwa, tafuta kuirejesha haraka iwezekanavyo. Unaposhika maagano yako, ikijumuisha fursa takatifu ya kuvaa gamenti kama ilivyoelekezwa katika ibada za mwanzo, utakuwa na ufikiaji mkubwa wa rehema, ulinzi, nguvu na uwezo wa Mwokozi.”(Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 26.3.3.2).