Kuwaimarisha Waumini Wapya
Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubakia kwenye Njia ya Agano


“Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubakia kwenye Njia ya Agano,” Kuwasaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano (2020)

“Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubakia kwenye Njia ya Agano,” Kuwasaidia Waumini Wapya Kubakia kwenye Njia ya Agano

Kuwasaidia Waumini Wapya na Wanaorudi Kubakia kwenye Njia ya Agano

mvulana akibatizwa

Kabla ya Ubatizo

  • Je, wameanzisha urafiki na waumini?

  • Je, wanashiriki mahitaji yao na waumini? Je, wamejiunga na darasa la kujitegemea kama inahitajika?

  • Je, wanajifunza na kusali kuhusu injili ya Yesu Kristo?

  • Je, wamejifunza kuhusu mahekalu na familia za milele na kuanza kazi ya historia ya familia?

  • Je, wamepanga tarehe ya kufanya ubatizo na uthibitisho kwa ajili ya mababu zao waliofariki?

  • Je, wanakidhi vigezo vya ubatizo na uthibitisho?

  • Je, wanahudhuria mikutano ya sakramenti kila mara?

familia ikitazama kishikwambi

Punde baada ya Ubatizo au Kurudi Kanisani

  • Je, wanahisi kukubalika na kata?

  • Je, akina kaka au akina dada wahudumu wameanza kuwatunza?

  • Je, wanahudhuria mkutano wa sakramenti kila mara?

  • Je, waumini wanaume wanaostahili wamepokea Ukuhani wa Haruni? Kama muumini wa kiume ni muumini anayerudi, je, hapo awali walipokea Ukuhani wa Haruni na Melkizedeki?

  • Je, wamepokea kibali cha hekalu kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho kwa ajili ya wafu (kama wanastahili) na kushiriki katika ibada hizo kwa ajili ya mababu zao waliofariki?

  • Je, wanaendelea kusali na kujifunza injili ya Yesu Kristo na kuungwa mkono na waumini na wamisionari?

  • Je, wamepokea jukumu Kanisani au jukumu la kuhudumu?

  • Je, wameshiriki katika darasa la kujitegemea kama inahitajika?

wanawake wakitabasamu

Ndani ya Mwaka wa Kwanza wa Ubatizo au Kurudi Kanisani

  • Je, wamekuza urafiki wa kudumu na waumini wa kata?

  • Je, wameimarisha imani yao katika Yesu Kristo kupitia sala na kujifunza injili kwa uthabiti?

  • Je, waumini wanaume wanaostahili wamepokea Ukuhani wa Melkidezeki?

  • Je, wanatoa huduma kwa wale walio na mahitaji? Je, wana wito wa Kanisa?

  • Je, wamepanga tarehe ya kupokea ibada zao wenyewe za hekaluni au kurudi hekaluni kufanya ibada kwa ajili ya mababu waliofariki? Je, wanaendelea kufanya kazi ya hekalu na historia ya familia?