Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Unataka Kuwa na Furaha Zaidi? Jaribu Shukrani
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Februari 2026


Ujumbe wa kila mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Februari 2026

Unataka Kuwa na Furaha Zaidi? Jaribu Shukrani

Wakati maisha yako yamejaa mabadiliko, shukrani inaweza kukusaidia kufokasi kwenye chanya na kubakia mwenye matumaini.

mtu chini ya mawingu ya mvua na mtu aliyezungukwa na ndege na vipepeo na maua

Vielelezo na Maggie Stephenson

Furaha yako itakuwa sawa na shukrani yako.”

Kama vile nukuu hii kutoka kwa Mzee Gary B. Sabin wa Sabini inavyopendekeza, wingi wa furaha unahusishwa moja kwa moja na jinsi ulivyo na shukrani. Inaleta maana—unapokuwa na shukrani, unafokasi kwenye vitu chanya badala ya vitu hasi.

Bado, maisha hayaendi kila mara kama yalivyopangwa. Mabadiliko yasiyotarajiwa yanaweza kukufanya uwe na msongo zaidi wa mawazo, huzuni au kuchanganyikiwa kuliko furaha. Lakini wakati mambo ni magumu, shukrani inaweza kukusaidia kubaki mwenye tumaini. Jaribu njia hizi tatu ili kuleta shukrani zaidi katika maisha yako.

1. Tafuta Mema

Mara nyingi, ni vigumu sana kuwa na shukrani wakati unahisi kama unapungukiwa na kitu. Lakini ni baraka zipi yawezekana unazipuuza kwa kufokasi kwenye kile ambacho huna badala ya kile ulichonacho?

Unapotafuta mazuri katika maisha yako, baada ya muda itakuwa rahisi kuyapata.

2. Toa Shukrani kwa Mtoaji

Unapohesabu baraka zako, usisahau kule zinapotoka.

Kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa zawadi Zake—ikijumuisha zawadi ya Mwana Wake—inaweza kuongeza upendo wako Kwake na imani katika Yeye. Rais D. Todd Christofferson, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, pia alielezea, “Hisia na kuonyesha shukrani kwa Mungu … huleta kuabudu kwa hisia ya kufanywa upya kwa shangwe,” ikikuletea shangwe na nguvu na kusaidia ushuhuda wako kubaki salama.

3. Fokasi kwenye Mpango wa Baba wa Mbinguni

Ni wazi, kuwa na shukrani haimaanishi kupuuza mambo magumu katika maisha au kuhisi furaha wakati wote. Hata Yesu Kristo alihisi na kukiri maumivu (ona Alma 7:11; Mafundisho na Maagano 19:18–19). Huzuni ni sehemu ya kawaida ya maisha ya duniani.

Lakini bila kujali chochote, kitu kimoja ambacho hakibadiliki kamwe: Mpango wa rehema wa Baba wa Mbinguni. Huzuni yote na maumivu unayopitia katika maisha vitawekwa sawa kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake (ona Ufunuo 21:4).

Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza: “Kuwa na shukrani wakati wa nyakati za dhiki haina maana kwamba tunapendezwa na hali zetu. Ina maana kwamba kupitia macho ya imani tunatazama zaidi ya changamoto zetu za sasa.”