"Pasaka," Rafiki, Aprili 2026, 46–48.
Ujumbe wa kila mwezi wa Rafiki, Aprili 2026
Pasaka
Musa alikwenda kwa Farao na kumwomba awaache huru watumwa wa Kiisraeli. Farao alikataa. Bwana alituma mapigo Misri, lakini Farao bado alisema hapana.
Bwana alisema angetuma pigo moja la mwisho. Mtoto mzaliwa wa kwanza wa kila familia huko Misri angekufa. Lakini kama Waisraeli wangefuata maelekezo Yake, pigo lingewapita.
Bwana aliwaambia Waisraeli kutoa dhabihu ya mwanakondoo dume mkamilifu na kupaka damu ya mwanakondoo juu ya milango yao.
Pigo likaja. Wazaliwa wote wa kwanza wa Wamisri walikufa, ikijumuisha mwana wa Farao. Lakini wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli waliokolewa kwa sababu walimtii Bwana.
Farao alimwambia Musa na Waisraeli waondoke Misri. Lakini Farao alikasirika. Yeye na jeshi lake waliwafuta.
Waisraeli walipiga kambi ufukoni mwa Bahari ya Shamu. Walipowaona Wamisri wakija, waliogopa. Musa alisema Bwana angewalinda.
Musa aliinua fimbo yake, na Bwana akaigawanya bahari. Waisraeli walivuka kwenye nchi kavu.
Wakati Waisraeli walipofika salama upande mwingine wa bahari, maji yalirudi na kuzamisha jeshi. Hatimaye Waisraeli walikuwa huru.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Yesu Kristo Alifufuka kwa ajili Yangu
Vielelezo na Audrey Day. Inaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.
Unaweza kufanya nini ili kumkumbuka Yesu Kristo Pasaka hii na mwaka mzima?
© 2026 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/19. Tafsiri iliidhinishwa: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, April 2026. Swahili. 20062 743