“Nuhu na Safina,” Rafiki, Februari 2026, 46–48.
Ujumbe wa kila mwezi wa Rafiki , Februari 2026
Nuhu na Safina
Nuhu na familia yake walimtii Bwana. Watu wengine wote walikuwa waovu sana. Bwana alimwambia Nuhu kwamba gharika ingeifunika dunia ikiwa watu hawakutubu.
Nuhu aliwaambia watu kwamba Bwana aliwapenda na aliwataka watubu na kuwa na imani katika Yesu Kristo. Watu hawakusikiliza.
Bwana alimwambia Nuhu kujenga meli kubwa iliyoitwa safina. Safina ingewaweka salama familia ya Nuhu wakati wa gharika.
Familia ya Nuhu iliingiza vyakula ndani ya safina. Bwana aliwapeleka angalau wanyama wawili wa kila aina kwa Nuhu ili awaingize ndani ya safina. Kisha mvua ikaanza kunyesha.
Mvua ilinyesha kwa siku 40 mchana na usiku 40. Gharika iliifunika dunia, kama vile Bwana alivyokuwa ameonya.
Familia ya Nuhu pamoja na wanyama wote ndani ya safina walielea kwa usalama juu ya maji.
Wakati gharika ilipokoma, safina ilisimama juu ya ardhi kavu. Nuhu na familia yake walimshukuru Bwana kwa kuwalinda. Bwana aliahidi kamwe kutoleta gharika duniani tena. Alituma upinde wa mvua kama ukumbusho wa ahadi Yake.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Kumfuata Nabii wa Bwana Kutanibariki
Kielelezo na Audrey Day
Je, unaweza kufanya nini ili kumfuata Nabii?
© 2026 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Translation of Monthly Friend Message, February 2026. Swahili. 19927 743