“Jela ya Liberty,” Rafiki, Agosti 2025, 26-28.
Ujumbe wa Kila Mwezi wa Rafiki , Agosti 2025
Jela ya Liberty
Watu wengi huko Missouri hawakuwapenda Watakatifu. Gavana aliwatuma askari ili kuwafanya waondoke.
Askari waliwakamata Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa. Usiku mmoja, walinzi walikuwa wakicheka kuhusu mambo mabaya waliyokuwa wamewafanyia Watakatifu.
Joseph alisimama wima na kuwanyamazisha kwa sauti kubwa, “Nyamazeni!” Yeye aliongea kwa nguvu za Mungu. Walinzi walisema samahani na kuacha kuzungumza.
Baadaye, Joseph na rafiki zake waliwekwa jela katika mji ulioitwa Liberty. Jela ilikuwa yenye baridi, ndogo, na yenye giza. Walikuwa tu na majani machafu ya kulalia. Chakula walichopewa kiliwafanya kuwa wagonjwa.
Joseph alikuwa na wasiwasi kuhusu Watakatifu. Lakini hangeweza kufanya cho chote cha kuwasaidia.
Joseph alisali sana. Aliuliza kama Mungu alikuwa amesahau kumhusu yeye na waumini wa Kanisa.
Mungu alijibu sala ya Joseph. Yeye alisema, “Mwanangu, amani iwe katika nafsi yako.” Mungu alimwambia Joseph kwamba changamoto zake hazitadumu milele, na zingekuwa kwa faida yake. Yeye aliahidi kwamba Yeye angekuwa pamoja na Joseph “milele na milele” (Mafundisho na Maagano 121:7, 46).
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Ninaweza Kuwa Kama Nuru kwa Wengine.
Kielelezo na Corey Egbert
Ni kwa jinsi gani wewe ni mfano mzuri kwa wengine?
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, August 2025. Swahili. 19642 743