Ujumbe wa kila mwezi wa Rafiki Juni 2025
Ujenzi wa Hekalu la Kirtland
Bwana alimwaambia Joseph Smith kwamba ulikuwa wakati wa kujenga hekalu huko Kirtland, Ohio, Marekani. Pangekuwa mahali maalum ambapo Bwana angewatembelea watu Wake na kufanya ahadi nao.
Watakatifu walianza kujenga hekalu. Iligharimu pesa nyingi na ilichukua kazi nyingi. Lakini walifurahishwa kupokea baraka za Bwana.
Watakatifu walipokuwa wakifanya kazi hekaluni, walianza kuishiwa pesa. Walisali kwa Mungu kwa ajili ya msaada.
Mwanamke aitwaye Caroline Tippets na familia yake walikuwa wamehifadhi pesa nyingi. Waliruhusu Kanisa kuazima pesa ili kusaidia kujenga hekalu.
Watakatifu walifanya kazi kwa bidii. Baadhi waliendesha mikokoteni iliyojaa mawe. Wengine walitengeneza nguo na chakula kwa ajili ya wafanyakazi.
Watoto walikusanya vipande vya vioo vilivyovunjika ili kusaga na kupaka kwenye kuta za hekalu ili ving’are katika mwanga wa jua.
Punde hekalu lilikamilika! Watakatifu walifurahia kwenda katika nyumba ya Bwana kupokea baraka alizowaahidi.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Bwana Anajua Mimi ni Nani na Ananipenda.
Kielelezo na Corey Egbert
Chora uso wako kwenye mviringo. Unajuaje kuwa Yesu Kristo anakupenda?
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa huko Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, June 2025. Swahili. 19643 743