“Joseph Smith Anapokea Mabamba ya Dhahabu,” Rafiki, Februari 2025, 26–28.
“Ninaweza Kuwa Shahidi Kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha Kweli,” Rafiki, Februari 2025, 48.
Ujumbe wa kila mwezi wa jarida la Rafiki, Februari 2025
Joseph Smith Anapokea Mabamba ya Dhahabu
Unaweza kusoma hadithi hii katika Joseph Smith—Historia ya 1:28–60.
Miaka mitatu baada ya Ono la Kwanza, Joseph Smith alijihisi vibaya kuhusu baadhi ya makosa aliyokuwa amefanya. Aliomba kwa Baba wa Mbinguni kuhusu hilo.
Wakati Joseph alipokuwa akisali, mwanga ulijaa chumbani. Alimwona malaika amesimama hewani. Jina la malaika yule lilikuwa Moroni.
Moroni alisema kulikuwa na kitabu kilichotengenezwa kwa kurasa za dhahabu, au mabamba. Kilizikwa katika kilima karibu na nyumbani kwao Joseph. Kitabu hicho kilihusu watu ambao waliishi katika mabara ya Amerika miaka mingi iliyopita. Moroni alisema Mungu angemsaidia Joseph kutafsiri kitabu hicho.
Joseph alikwenda kwenye kilima na kukuta mabamba hayo chini ya jiwe zito. Moroni alikuja na kusema kwamba Joseph bado hakuwa tayari kuyachukua.
Joseph alipokuwa mkubwa, Moroni alikutana naye juu ya kilima na kumpatia yale mabamba. Moroni alimwambia Joseph ayatunze salama.
Joseph alianza kutafsiri mabamba yale katika lugha ya Kiingereza. Alitumia vifaa maalumu kutoka kwa Mungu ili kumsaidia. Kitabu hicho kilichapishwa mwaka 1830 kama Kitabu cha Mormoni. Kinafundisha kuhusu Yesu Kristo na injili Yake.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Ninaweza Kuwa Shahidi Kwamba Kitabu cha Mormoni Ni cha Kweli.
Kielelezo na Corey Egbert
Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Yesu Kristo katika Kitabu cha Mormoni?
© 2025 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, February 2025. Swahili. 19641 743